Jimbo Kuu la Juba
Jimbo Kuu la Juba (kwa Kilatini Archidioecesis Iubaensis) ni mojawapo kati ya majimbo 7 ya Kanisa Katoliki nchini Sudan Kusini na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Chini yake kuna kanda ya Kanisa yenye majimbo yafuatayo: Malakal, Rumbek, Tombura-Yambio, Torit, Wau na Yei.
Askofu mkuu wake ni Stephen Ameyu Martin Mulla.
Historia
hariri- 1927: Kuanzishwa kwa Apostolic Prefecture ya Bahr el-Gebel
- 1951: Kupandishwa cheo kuwa Apostolic Vicariate
- 1974: Kufanywa jimbo kuu
Uongozi
haririViongozi wote wa jimbo mpaka leo wamepatikana katika shirika la Wamisionari la mtakatifu Daniel Comboni.
Takwimu
haririEneo la jimbo lina kilometa mraba 25,137, ambapo kati ya wakazi 945,000 (2013) Wakatoliki ni 745,000 (sawa na 78.8%). Parokia ziko 12, mapadri ni 60 na watawa 76,
Hati rasmi za Papa kwa Kilatini
hariri- (Kilatini) Breve Expedit ut, AAS 19 (1927), p. 405
- (Kilatini) Bolla Si uberes fructus, AAS 43 (1951), p. 583
- (Kilatini) Bolla Cum in Sudania, AAS 67 (1975), p. 164