14 Oktoba
tarehe
(Elekezwa kutoka Oktoba 14)
Sep - Oktoba - Nov | ||||||
1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 |
8 | 9 | 10 | 11 | 12 | 13 | 14 |
15 | 16 | 17 | 18 | 19 | 20 | 21 |
22 | 23 | 24 | 25 | 26 | 27 | 28 |
29 | 30 | 31 | ||||
Kalenda ya Gregori |
Tarehe 14 Oktoba ni siku ya 287 ya mwaka (ya 288 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 78.
Matukio
hariri- 1066 - Mapigano ya Hastings; jeshi lililochoka la Uingereza linashindwa na Wanormani chini ya William Mshindi. Uingereza unatekwa na Wanormani.
Waliozaliwa
hariri- 1890 - Dwight D. Eisenhower, Rais wa Marekani (1953-1961)
- 1894 - Edward Cummings, mwandishi kutoka Marekani
- 1914 - Raymond Davis, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 2002
- 1927 - Roger Moore, mwigizaji wa filamu kutoka Uingereza
- 1930 - Mobutu Sese Seko, Rais wa nchi ya Zaire
- 1950 - John Zefania Chiligati, mwanasiasa wa Tanzania na Waziri wa Ardhi (2005-2010)
- 1978 - Usher Raymond, mwanamuziki kutoka Marekani
Waliofariki
hariri- 1066 - Mfalme Harold wa Uingereza kwenye mapigano ya Hastings
- 1956 - Owen Davis, mwandishi kutoka Marekani
- 1984 - Martin Ryle, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1974
- 1999 - Julius Nyerere, Rais wa kwanza, "Mwalimu" na "Baba wa Taifa" wa Tanzania
- 2005 - Poxi Presha, mwanamuziki kutoka Kenya
Sikukuu
haririWakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Papa Kalisti I, Lupulo wa Capua, Gaudensi wa Rimini, Donasiani wa Reims, Fortunati wa Todi, Manekilde, Venansi wa Luni, Angadrisma, Dominiko Loricatus n.k.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu 14 Oktoba kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |