Wafa Mustafa

Mwandishi wa habari na mwanaharakati wa Syria

Wafa Mustafa (1989/1990 (umri 31–32) ) ni mwandishi wa habari wa nchini Syria na mwanaharakati ambaye hufanya kampeni ya kuachiliwa kwa wafungwa wa Syria . Kama mwanaharakati na mwanachama wa zamani wa Families for Freedom, Mustafa amelishawishi kwa kiasi kikubwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa wito wa kuachiliwa kwa majina na maeneo ya wale wote ambao mamlaka ya Syria inayo kifungoni. Anatoa wito kwa wafungwa wote nchini Syria kuachiliwa, iwe wanashikiliwa na utawala wa Assad au na makundi ya upinzani, ingawa pia anaunga mkono maandamano ya umma yaliyoanza mwaka 2011 dhidi ya serikali ya Bashar al-Assad .

Mustafa pia anafanya kampeni ya kutambuliwa kimataifa kwa wakimbizi wa Syria dhidi ya uhusiano wa kawaida wa kimataifa na serikali ya Assad.

Maisha ya awali

hariri

Mustafa alizaliwa huko Masyaf na yeye ndiye mkubwa kati ya mabinti watatu. Familia ya Mustafa ilikuwa inajishughulisha na shughuli za kisiasa na huria, na baba yake alimpeleka Wafa kwenye maandamano huko Damascus kuiunga mkono Palestina kuanzia akiwa na umri wa miaka 10. Mustafa aliandamana mbele ya ubalozi wa Libya mwanzoni mwa Vita vya kwanza vya wenyewe kwa wenyewe vya Libya, na mamlaka ya Syria ilipowashambulia waandamanaji na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria vikaanza, alihusika katika maandamano.

Maisha binafsi

hariri

Mnamo Julai 2013, Mustafa aligunduliwa kuwa na matatizo ya Anxiety sugu na depression . Mwaka huo, baada ya kifo cha rafiki yake wa karibu, alijiweka ndani ya nyumba yake kwa muda wa miezi mitatu, bila kutoka nje ya chumba chake isipokuwa labda kwenda bafuni, ambapo ilimsababisha kupoteza uzito sana. Mwishowe mpaka baba yake alipomshawishi hatimaye kutafuta matibabu.

Mustafa, mama yake, na dada yake walikimbia Syria kwa muda wa wiki moja baada ya baba yake Ali kukamatwa mnamo Julai 2013, wakihofia wao pia kukamatwa. [1] Waliishi Uturuki kwa miaka 3, wakikabiliwa na umaskini, kwani walikuwa wamechukua pasipoti zao tu. [2] Wafa kwa sasa anaishi Berlin, na alihitimu kutoka Chuo cha Bard Berlin mnamo mwaka 2020 akiwa na shahada ya ubinadamu na sanaa. [1]

Mustafa bado anaichukulia Syria kama makazi yake, na anapanga kurejea iwapo utawala wa Assad utaanguka.

Uanaharakati

hariri

Kutoweka kwa Ali Mustafa

hariri

Mustafa anatajwa kama mshawishi wa uanaharakati wake kwa kutoweka kwa baba yake, Ali Mustafa, mwanaharakati wa haki za binadamu, [2] ambaye alionekana kwa mara ya mwisho tarehe 2 Julai 2013. Siku hiyo, Wafa anasimulia mashahidi wakisema kwamba kundi la wanaume lilishambulia nyumba ya familia yake, ambako alikuwa ameishi kwa miezi miwili tangu kifo cha rafiki yake wa karibu katika shambulio la roketi.

Ali alinyanyaswa mwanzoni mwa mwaka 2011 na Usalama wa Taifa, ambapo alikamatwa mara nyingi kabla na baada ya mapinduzi, pamoja na mwenzake Hussam al-Dhafri na watu wenye silaha waliovalia nguo za kiraia mwanzoni mwa maandamano ya serikali mwezi Machi 2011. Hussam alifariki kutokana na mateso katika mojawapo ya vituo vya vizuizi vya serikali.

Kukamatwa

hariri

Mnamo Septemba 2011, Mustafa alikamatwa na kuzuiliwa huko Damascus, Wakati huo alikuwa mwanafunzi wa uandishi wa habari na vyombo vya habari. lakini baada ya kukamatwa, jina lake liliwekwa kwenye orodha nyeusi ya umma na hivyo alilazimika kuacha elimu yake. Baada ya kuwasili Ujerumani mnamo mwaka 2016. Mustafa aliendelea na masomo yake katika Chuo cha Bard Berlin ambako alihitimu katika programu ya HAST.

Kazi ya Uanaharakati

hariri

Leo, Wafa Mustafa anafanya kazi ya kupata taarifa zozote za kuhusu baba yake na wakimbizi wengine waliozuiliwa. Alijiunga na Families for Freedom mnamo 2018 hadi mwaka wa 2021. [3]

Mnamo tarehe 30 Mei 2020, Mustafa aliandamana kwa amani nje ya mahakama huko Koblenz, Ujerumani eneo la kesi ya Al Khatib, afisa mkuu wa zamani wa ujasusi wa jeshi la Syria, na mshirika wake anayedaiwa kuwa ni Eyad Al-Gharib walikabiliwa na kesi nchini Ujerumani chini ya kanuni ya kisheria ya mamlaka ya ulimwengu kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu . Walishtakiwa kwa kusimamia mauaji 58 na mateso ya wengine 4,000 katika kituo cha kizuizi cha Damascus . Alisambaza picha 61 za wafungwa, pamoja na picha ya baba yake. [1] Kesi ilifunguliwa na mwendesha mashtaka mkuu wa shirikisho la Ujerumani dhidi ya wanachama wawili wa zamani wa vyombo vya usalama vya Rais Bashar Al Assad. [4]

Mnamo 23 Julai 2020, Mustafa alitoa taarifa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kulazimishwa kutoweka na kuwekwa kwa vizuizi nchini Syria. [3]


Marejeo

hariri
  1. "'My dad went missing eight years ago – I will never stop searching for answers'", 17 March 2021. (en) 
  2. "One woman's campaign for Syria's disappeared people", 15 March 2021. (en) 
  3. 3.0 3.1 "Briefing to the UN Security Council by Wafa Mustafa". The Syria Diary (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-05-15."Briefing to the UN Security Council by Wafa Mustafa".
  4. Schmitz-Buhl, Lina (27 Januari 2021). "Enforced disappearances in Syria and the Al Khatib trial in Germany". voelkerrechtsblog.org (kwa Kiingereza). doi:10.17176/20210127-191051-0. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 13 Machi 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)