Jimbo Kuu la Dodoma
(Elekezwa kutoka Jimbo Katoliki la Dodoma)
Jimbo Kuu la Dodoma (kwa Kilatini Archidioecesis Dodomaensis) ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Kikanisa lina majimbo ya Kondoa na Singida chini yake.
Askofu mkuu wake ni Beatus Kinyaiya, O.F.M.Cap..
Historia
hariri- 1935: Kuanzishwa kwa Apostolic Prefecture ya Dodoma kutokana na Apostolic Vicariate ya Bagamoyo
- 1951: Kupandishwa cheo kuwa Apostolic Vicariate ya Dodoma
- 1953: Kufanywa dayosisi
- 6 Novemba 2014: Kupandishwa cheo na kuwa jimbo kuu.
Uongozi
hariri- Maaskofu wakuu wa Dodoma
- Beatus Kinyaiya, O.F.M.Cap.
- Maaskofu wa Dodoma
- Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga (2011-2013)
- Jude Thadaeus Ruwa’ichi OFMCap (2005 – 2010)
- Matthias Joseph Isuja (1972 – 2005)
- Anthony Jeremiah Pesce CP (1953 – 1971)
- Vicar Apostolic wa Dodoma
- Anthony Jeremiah Pesce CP (1951 – 1953)
- Prefect Apostolic wa Dodoma
- Padri Stanislao dell’Addolorata CP (1937 – 1941)
Takwimu
haririEneo ni la kilometa mraba 41,311, ambapo kati ya wakazi 1,908,000 (2006) Wakatoliki ni 398,000 (20.9%).