Jimbo Katoliki la Machakos
Jimbo Katoliki la Machakos ni mojawapo kati ya majimbo 27 ya Kanisa Katoliki nchini Kenya.
Liko chini ya jimbo kuu la Nairobi.
Baada ya kumegwa tarehe 22 Julai 2023 ili kuzaa Jimbo Katoliki la Wote, limebaki na eneo la km2 6,126, Wakatoliki 610,150 kati ya wakazi 1,421,932, parokia 49, mapadri 112 wanajimbo na 22 wamisionari, mashemasi 6, waseminari 33 na makatekista 928.
Askofu ana makao makuu mjini Machakos.
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Machakos kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |