Kanisa Katoliki la Kisiria la Malankara

Kanisa Katoliki la Kisiria la Malankara (kwa Kimalayalam: മലങ്കര സുറിയാനി കത്തോലിക്കാ സഭ) ni mojawapo kati ya madhehebu ya Ukristo wa mashariki yenye ushirika kamili na Papa na Kanisa Katoliki lote.

Qurbono, yaani liturujia ya Kimungu inavyoadhimishwa na Wamalankara.
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo

Papa: Fransisko
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Liturujia ya Trento Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Linafuata mapokeo ya Antiokia na kutumia liturujia ya Antiokia, lakini linapatikana hasa India kusini na katika nchi walipohamia watu wa eneo hilo, kama vile Uarabuni, Uingereza, Marekani.

Kwa jumla lina waamini 450,000 hivi, kutokana na 5 tu wa kwanza waliojiunga rasmi na Kanisa Katoliki tarehe 30 Septemba 1930 chini ya askofu mkuu Mar Ivanios Geevarghese, wengine wakiwa Askofu Jacob Mar Theophilos, padri John Kuzhinapurath OIC, shemasi Alexander OIC, na mlei Chacko Kilileth.

Majimbo ni 11 nchini India na 1 Marekani, na mapadri ni 639.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
  Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanisa Katoliki la Kisiria la Malankara kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.