Ugiriki
Ugiriki (pia: Uyunani; kwa Kigiriki: Ελλάδα, Ellada, au Ελλάς, Ellas) ni nchi ya Ulaya Kusini-Mashariki katika kusini ya rasi ya Balkani.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Ελευθερία ή Θάνατος (Eleftheria i thanatos - "Uhuru au mauti") | |||||
Wimbo wa taifa: Ύμνος εις την Ελευθερίαν - "Wimbo la Uhuru" | |||||
![]() | |||||
Mji mkuu | Athens | ||||
Mji mkubwa nchini | Athens | ||||
Lugha rasmi | Kigiriki | ||||
Serikali | Jamhuri Katerina Sakellaropoulou (Κατερίνα Σακελλαροπούλου) Kyriakos Mitsotakis (Κυριάκος Μητσοτάκης) | ||||
Uhuru Ilitangazwa Ilitambuliwa |
25 Machi 1821 1829 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
131,990 km² (ya 96) 0.8669 | ||||
Idadi ya watu - 2005 kadirio - 2012 sensa - Msongamano wa watu |
11,244,118 (ya 74) 10,816,286 77/km² (ya 120) | ||||
Fedha | Euro (€)2 (EUR )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
EET (UTC+2) EEST (UTC+3) | ||||
Intaneti TLD | .gr 3 | ||||
Kodi ya simu | +30
- | ||||
1 Wananchi walikataza kurudi kwa ufalme tar. 8 Desemba 1974. 2 Prior to 2001: Greek Drachma. |
Imepakana na Albania, Masedonia Kaskazini, Bulgaria na Uturuki.
Upande wa kusini-magharibi na kusini-mashariki kuna pwani ndefu kwenye Bahari ya Mediteranea.
Nchi hiyo iko kwenye upande wa kusini wa Rasi ya Balkani. Kijiografia huwa na sehemu za Ugiriki bara, rasi ya Peloponesi upande wa kusini inayounganishwa kwa shingo ya nchi nyembamba, halafu visiwa vingi upande wa Bahari ya Aegean, Bahari ya Adria na kwenye Mediteranea yenyewe. Visiwa vikubwa zaidi ni Kreta, Euboea, Lesbos na Rhodos.
Ugiriki ni nchi yenye historia ndefu na maarufu sana, hata inaitwa "nchi mama ya Ulaya".
Lugha ya Kigiriki inaendelea kuandikwa kwa Alfabeti ya Kigiriki inaotumiwa tangu miaka 3000 iliyopita, lakini lugha yenyewe imebadilika. Wagiriki wa leo hawaelewi tena Kigiriki cha Kale moja kwa moja.
Wakazi wengi wanafuata dini ya Ukristo, hasa katika Kanisa la Kiorthodoksi la Kigiriki (97%). 1.3% ni Waislamu.
Ugiriki ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu 1981.
Tazama piaEdit
Viungo vya njeEdit
- (Kiingereza) (Kifaransa) (Kigiriki) Rais wa Ugiriki
Nchi za Umoja wa Ulaya | |
---|---|
Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Hispania | Hungaria | Ireland | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ugiriki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |