Makundinyota 88 ya UKIA

orodha ya makala za Wikimedia
(Elekezwa kutoka Kundinyota 88 za UKIA)

Kuhusu makundinyota kwa jumla na historia yao tazama makala Kundinyota

Mpangilio wa anga lote kwa makundinyota kufuatana na Delporte na Ukia

Makundinyota 88 ya UKIA ni jinsi gani Umoja wa Kimataifa ya Astronomia (UKIA) uliamua kupanga tufe la anga kwa kusudi la kutaja mahali pa nyota jinsi inayoonekana kwenye anga. Kuna mpangilio tofauti wa nyota kwa makundi katika tamaduni mbalimbali duniani.

Hapo chini inafuata orodha ya makundinyota 88 yaliyoamuliwa na Umoja wa Kimataifa ya Astronomia (UKIA) kwa upimaji wa anga lote. Kwa historia ya upangaji huu angalia makala ya Kundinyota.

UKIA ulichagua majina kutoka lugha ya Kilatini[1] ambayo yanarejelea mara nyingi hadithi za mitholojia ya Ugiriki wa Kale.

Chanzo cha majina ya Kiswahili mara nyingi ni kawaida ya mabaharia Waswahili waliotafuta njia zao wakati wa usiku kwenye Bahari ya Hindi kwa msaada wa nyota. Idadi kubwa ya majina haya yalipokelewa kutoka kwa Kiarabu ilhali Waarabu wenyewe walitumia makundinyota 48 waliyowahi kupokea kutoka kwa Wagiriki wa Kale jinsi zilivyotajwa katika kitabu cha Almagesti cha Ptolemaio.[2]

Majina ya Kiswahili kwa makundinyota 49 (pamoja na majina ya nyota 45) yalikusanywa na mwanaisimu Mholanzi Jan Knappert[3] na kuhifadhiwa hata kama sehemu kubwa ya elimu hii imeshapotea kwa wenyeji kutokana na mabadiliko ya teknolojia maana leo hii mabaharia hawatumii tena nyota. Majina mengine yalitafsiriwa kutoka Kilatini cha kimataifa kwa Kiswahili.

Makundinyota 12 ni sehemu ya Zodiaki inayotumiwa pia na wanajimu kwa kutabiri tabia za mtu na heri zake. Kwa tisa ya makundinyota haya wanajimu walianza kutumia majina mbadala kwa kutafsiri kutoka kawaida ya Kiingereza au kwa kutaja nembo ya kundinyota. Jedwali inaonyesha majina mbdala za wanajimu kwa mabano yenye alama ya *.

Jedwali ya makundinyota 88 kufuatana na jina la UKIA

(Unaweza kupanga kila nguzo ya jedwali kufuatana na a-b-c)

Jina la Kiswahili Jina la Kilatini
(la kimataifa)
Chanzo cha
jina la Kiswahili
Mara (lat.: Andromeda) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Pampu (lat.: Antlia) (limetafsiriwa)
Ndege wa Peponi (lat.: Apus) (limetafsiriwa)
Ndoo *(Dalu) (lat.: Aquarius) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Ukabu (lat.: Aquila) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Madhabahu (lat.: Ara) (limetafsiriwa)
Kondoo *(Hamali) (lat.: Aries) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Hudhi (lat.: Auriga) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Bakari (lat.: Boötes) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Patasi (lat.: Caelum) (limetafsiriwa)
Twiga (lat.: Camelopardalis) (limetafsiriwa)
Nge *(Saratani) (lat.: Cancer) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Mbwa wawindaji (lat.: Canes Venatici) (limetafsiriwa)
Mbwa Mkubwa (lat.: Canis Major) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Mbwa Mdogo (lat.: Canis Minor) (limetafsiriwa)
Mbuzi *(Jadi) (lat.: Capricornus) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Mkuku (lat.: Carina) (limetafsiriwa)
Mke wa Kurusi (lat.: Cassiopeia) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Kantarusi (lat.: Centaurus) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Kifausi (lat.: Cepheus) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Ketusi (lat.: Cetus) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Kinyonga (lat.: Chamaeleon) (limetafsiriwa)
Bikari (lat.: Circinus) (limetafsiriwa)
Njiwa (lat.: Columba) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Nywele za Berenike (lat.: Coma Berenices) (limetafsiriwa)
Kobe (lat.: Corona Australis) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Kasi ya Masakini (lat.: Corona Borealis) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Ghurabu (lat.: Corvus) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Batiya (lat.: Crater) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Salibu (lat.: Crux) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Dajaja (lat.: Cygnus) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Dalufnin (lat.: Delphinus) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Panji (lat.: Dorado) (limetafsiriwa)
Tinini (lat.: Draco) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Mwanafarasi (lat.: Equuleus) (limetafsiriwa)
Nahari (lat.: Eridanus) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Tanuri (lat.: Fornax) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Mapacha *(Jauza) (lat.: Gemini) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Kuruki (lat.: Grus) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Rakisi (lat.: Hercules) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Saa (lat.: Horologium) (limetafsiriwa)
Shuja (lat.: Hydra) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Nyoka Maji (lat.: Hydrus) (limetafsiriwa)
Mhindi (lat.: Indus) (limetafsiriwa)
Mjusi (lat.: Lacerta) (limetafsiriwa)
Simba *(Asadi) (lat.: Leo) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Simba Mdogo (lat.: Leo Minor) (limetafsiriwa)
Arinabu (lat.: Lepus) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Mizani (lat.: Libra) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Dhibu (lat.: Lupus) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Washaki (lat.: Lynx) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Shaliaki (lat.: Lyra) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Meza (lat.: Mensa) (limetafsiriwa)
Hadubini (lat.: Microscopium) (limetafsiriwa)
Munukero (lat.: Monoceros) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Nzi (lat.: Musca) (limetafsiriwa)
Pembemraba (lat.: Norma) (limetafsiriwa)
Thumni (lat.: Octans) (limetafsiriwa)
Hawaa (lat.: Ophiuchus) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Jabari (lat.: Orion) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Tausi (lat.: Pavo) (limetafsiriwa)
Farasi (lat.: Pegasus) (limetafsiriwa)
Farisi (lat.: Perseus) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Zoraki (lat.: Phoenix) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Mchoraji (lat.: Pictor) (limetafsiriwa)
Samaki *(Hutu) (lat.: Pisces) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Hutu Junubi (lat.: Piscis Austrinus) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Shetri (lat.: Puppis) (limetafsiriwa)
Dira (lat.: Pyxis) (limetafsiriwa)
Nyavu (lat.: Reticulum) (limetafsiriwa)
Sagita (lat.: Sagitta) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Mshale *(Kausi) (lat.: Sagittarius) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Nge *(Akarabu) (lat.: Scorpius) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Najari (lat.: Sculptor) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Ngao (lat.: Scutum) (limetafsiriwa)
Hayya (lat.: Serpens) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Sudusi (lat.: Sextans) (limetafsiriwa)
Ng'ombe *(Tauri) (lat.: Taurus) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Darubini (lat.: Telescopium) (limetafsiriwa)
Pembetatu (lat.: Triangulum) (limetafsiriwa)
Pembetatu ya Kusini (lat.: Triangulum Australe) (limetafsiriwa)
Tukani (lat.: Tucana) (limetafsiriwa)
Dubu Mkubwa (lat.: Ursa Major) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Dubu Mdogo (lat.: Ursa Minor) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Tanga (lat.: Vela) (limetafsiriwa)
Mashuke *(Nadhifa) (lat.: Virgo) Mabaharia Waswahili (Knappert)
Panzimaji (lat.: Volans) (limetafsiriwa)
Mbweha (lat.: Vulpecula) Mabaharia Waswahili (Knappert)

Marejeo

  1. Wakati wa kutokea kwa astronomia ya kisasa ya karne ya 17 katika Ulaya hii lugha ya Kilatini ilikuwa lugha ya kimataifa ya sayansi.
  2. Makundinyota mengine yaliongezwa baadaye na wataalamu kutoka nchi za Ulaya, soma historia ya kundinyota.
  3. Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331