Jamhuri ya Afrika ya Kati

(Elekezwa kutoka Afrika ya Kati (Jamhuri ya))
Jamhuri ya Afrika ya Kati (Kiswahili)
Ködörösêse tî Bêafrîka (Kisango)
Bendera ya Jamhuri ya Afrika ya Kati Nembo ya Jamhuri ya Afrika ya Kati
(Bendera ya Jamhuri ya Afrika ya Kati) (Nembo ya Jamhuri ya Afrika ya Kati)
Lugha rasmi Kisango, Kifaransa
Mji Mkuu Bangui
Mji Mkubwa Bangui
Serikali Jamhuri
Rais Faustin-Archange Touadéra
Eneo km² 622,984
Idadi ya wakazi 3,895,139 (2018)
Wakazi kwa km² 6.25
Uchumi nominal Bilioni $2.003
Pesa CFA frank (XFA) (Frank ya Afrika ya Kati)
Kaulimbiu "Umoja, Heshima, Kazi"
Wimbo wa Taifa E Zingo (Uamsho mpya)
Jamhuri ya Afrika ya Kati katika Afrika

Jamhuri ya Afrika ya Kati (kwa Kisango Ködörösêse tî Bêafrîka) ni nchi ya bara bila pwani katika Afrika ya Kati.

Imepakana na Chadi upande wa kaskazini, Sudan na Sudan Kusini upande wa mashariki, Jamhuri ya Kongo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa kusini na Kamerun upande wa magharibi.

Jiografia

hariri
 
Ramani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati

Nchi hii, hasa inashikilia mbuga ya Sudani-Guinea, lakini pia jangwa la Sahara upande wa kaskazini na msitu wa ikweta kusini.

Theluthi mbili za eneo la nchi zimetapakaa kwa mabia ya mto Ubangi unaotiririka kusini kwa Mto Kongo, na theluthi ya eneo katapakaa kwa mabia ya mto Shari, unaotiririka kusini kwa Ziwa Chadi.

Historia

hariri

Historia ya Kale

hariri

Ukoloni wa Ufaransa

hariri

Kwa sababu ya utapakazi wa eneo kwa mabia ya mto Ubangi na mto Shari, Wafaransa wakati wa ukoloni waliita nchi hii Ubangi-Shari (Oubangui-Chari kwa Kifaransa).

Ilipokuwa koloni la Ufaransa, Ubangi-Shari ziliwekewa mamlaka ya madaraka kama eneo la Jamii ya Wafaransa mwaka wa 1958, lakini baadaye ilipata uhuru tarehe 13 Agosti 1960.

Kwa miongo mitatu kutoka uhuru, ‘Jamhuri ya Afrika ya Kati’ ilitawaliwa na serikali za mabavu zilizonyakua mamlaka bila kufuata taratibu za demokrasia.

Kwa namna ya pekee Jean-Bédel Bokassa alitawala kuanzia tarehe 31 Desemba 1965 hadi Septemba 1979, akijifanya kaisari tarehe 4 Desemba 1976.

Mwaka wa 1993, kura za kidemokrasia za kwanza zilifanywa na kumchagua Ange-Félix Patassé kuwa Rais. Lakini Rais Patassé alipinduliwa na Jenerali François Bozizé mwaka wa 2003. Baadaye huyo alishinda uchaguzi mnamo Mei 2005 na kuiongoza nchi mpaka Machi 2013 alipolazimika kukimbia.

Kati ya Novemba 2012 na tarehe 23 Julai 2014 vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipamba kwa ukatili na vinaendelea hadi mwaka 2020.

Jamhuri ya Afrika ya Kati imegawiwa katika maeneo 14, yanayoitwa préfectures, na pia maeneo 2 ya uchumi (préfectures economique) na mji mmoja (commune).

Maeneo hayo yamegawiwa zaidi katika wilaya 71 zinazoitwa sous-préfectures.

mikoa ni: Bamingui-Bangoran, Basse-Kotto, Haute-Kotto, Haut-Mbomou, Kémo, Lobaye, Mambéré-Kadéï, Mbomou, Nana-Mambéré, Ombella-M'Poko, Ouaka, Ouham, Ouham-Pendé, na Vakaga; maeneo ya uchumi ni Nana-Grébizi na Sangha-Mbaéré; na mji ni Bangui.

 
Kanisa la vijijini huko Niem.

Nchi ina watu 4,666,368 waliogawanyika katika makabila 80, kila moja likiwa na lugha ya pekee. Ile inayowaunganisha katika mawasiliano ni Kisango, ambacho ni lugha rasmi pamoja na Kifaransa.

Kadiri ya sensa ya mwaka 2003, kati ya wakazi, 80.3% ni Wakristo (51.4% Waprotestanti na 28.9% Wakatoliki). Waislamu ni 10% na wengi wa waliobaki wanafuata dini za jadi.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons


Habari

hariri

Uchambuzi

hariri

Maelekezo

hariri

Makabila na koo

hariri
  • African Pygmies Utamaduni na muziki wa watu wa Jamhuri ya Afrika, picha na ulezaji wa ukoo.


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Afrika ya Kati kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.