Morisi ni nchi inayoitwa rasmi Jamhuri ya Morisi (kwa Kiingereza: Republic of Mauritius, kwa Kifaransa: République de Maurice). Ni nchi ya visiwa katika Bahari Hindi karibu na Afrika, takriban Km 900 mashariki kwa Madagaska na km 4000 kusini-magharibi kwa Bara Hindi.

Republic of Mauritius
République de Maurice
Bendera ya Mauritius Nembo ya Mauritius
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Stella Clavisque Maris Indici
(Kilatini: Nyota na ufunguo wa Bahari Hindi)
Wimbo wa taifa: Taifa
Lokeshen ya Mauritius
Mji mkuu Port Louis
20°10′ S 57°31′ E
Mji mkubwa nchini Port Louis
Lugha rasmi Kiingereza na Kifaransa ingawa si rasmi kabisa
Serikali Jamhuri
Prithvirajsing Roopun
Pravind Jugnauth
Uhuru
kutoka Uingereza
12.03.1968
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
2,040 km² (ya 169)
0.05
Idadi ya watu
 - Julai 2019 kadirio
 - 2013 sensa
 - Msongamano wa watu
 
1,265,475 (ya 156)
1,259,838
618/km² (ya 19)
Fedha Mauritian Rupee (MUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+4)
(UTC)
Intaneti TLD .mu
Kodi ya simu +230

-


Ramani ya kisiwa cha Morisi

Nchi ilipata uhuru tarehe 12 Machi 1968, ikawa jamhuri tarehe hiyohiyo mwaka 1992.

Jina linatokana na kisiwa chake kikubwa, lakini eneo la jamhuri ni pamoja na kisiwa cha Rodrigues, visiwa vidogo vya Cargados Carajos na Agalega.

Hivyo vyote ni sehemu ya funguvisiwa la Maskarena pamoja na kisiwa cha Réunion ambacho ni mkoa wa Ufaransa.

Mji mkuu wa jamhuri ni Port Louis.

Eneo la Jamhuri ya Morisi

hariri

Visiwa vya jamhuri vimesambaa katika eneo pana sana:

Kisiwa kikuu cha Mauritius ni km² 1,865 au 91% za ardhi yote ya jamhuri. Karibu wakazi wote (1,261,208) huishi huko.

Kisiwa cha Rodrigues kipo km 560 mashariki kwa Morisi yenyewe. Eneo lake ni km² 109; kuna wakazi 41,000.

 
Visiwa vya Makarena kati ya visiwa vya Kiafrika katika Bahari Hindi

Visiwa vya Cargados Carajos (vinaitwa pia Saint Brandon) ni visiwa 16 vidogo sana, vyenye eneo la km² 1.3 pekee. Viko km 300 kaskazini kwa Morisi. Kuna wakazi mia chache wavuvi.

Agalega ni visiwa viwili, yaani Kisiwa cha Kaskazini na Kisiwa cha Kusini, takriban km 1,122 kaskazini kwa Morisi yenyewe. Visiwa hivyo vina eneo la km² 70. Kuna vijiji vya Vingt Cinq na La Fourche kwenye kisiwa cha kaskazini na kijiji cha Ste Rita kwenye kisiwa cha kusini. Wenyeji wanalima mazao ya mnazi pamoja na mboga kwa matumizi yao wenyewe.

Wakazi

hariri

Watu wa Morisi ni mchanganyiko mkubwa kutokana na historia ya visiwa hivyo.

Baada ya Waarabu na Wareno kuvumbua Morisi, wakazi wa kwanza (1638) walikuwa Waholanzi, lakini hawakuacha dalili isipokuwa majina ya mahali kwa sababu waliondoka mwaka 1710 baada ya kushindwa kiuchumi.

Wafaransa walitawala visiwa kati ya 1715 hadi 1810. Walianzisha miji na mashamba ya miwa. Nje ya walowezi, Wafaransa walipeleka pia watumwa kutoka bara la Afrika. Mwaka 1767 walikuwepo Wafaransa 3,163 pamoja na watumwa Waafrika 15,000, pia Wahindi 587.

Uingereza ulichukua utawala wa visiwa mwaka 1810 katika vita dhidi ya Napoleon. Siku zile Kiingereza kilikuwa lugha rasmi ya serikali, lakini wakazi waliendelea kutumia lahaja za Kifaransa.

Baada ya kuwapatia watumwa uhuru, Waingereza walileta Wahindi wengi, baadaye pia Wachina kama wafanyakazi kwenye mashamba ya sukari. Leo hii idadi kubwa ya wakazi ni wa asili ya Uhindi (67%), wakifuatwa na Waafrika (28%), Wachina (3%) na Wafaransa (2%).

Lakini 90% ya wananchi hutumia krioli ya Kimorisyen (aina ya Kifaransa) kama lugha ya kwanza. Asilimia 5 hutumia Kibhojpuri au lugha za Uhindi kama vile Kiurdu, Kitamil. Asilimia 4.4 hutumia Kifaransa, na 0.6% tu Kiingereza.

Karibu nusu (47.9%) ya wakazi hufuata dini ya Uhindu, 32.3% Ukristo (hasa wa Kanisa Katoliki) na 18.2% ni Waislamu (hasa Wasunni, lakini pia Washia).

Uchumi

hariri

Hadi leo kilimo cha miwa (sukari) ni uti wa mgongo wa uchumi wa Morisi.

Nchi iliendelea kuwa na serikali zilizochaguliwa bila kupinduliwa: hali hii ya utulivu ilisaidia kukua kwa uchumi. Hali ya maisha ni ya juu kuliko nchi nyingi za Afrika.

Tazama pia

hariri


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Morisi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.