Orodha ya Marais wa Marekani

(Elekezwa kutoka Marais wa Amerika)

Katika Katiba ya Marekani, Rais wa Marekani ni Mkuu wa Taifa pamoja na kuwa Mkuu wa Serikali wa nchi hiyo. Kama mkuu wa tawi la utendaji na mkuu wa serikali ya majimbo, rais ndiye mwenye cheo na madaraka makuu zaidi katika nchi ya Marekani. Rais pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Marekani. Kuchaguliwa kwa rais wa Marekani ni kupitia mfumo wa wawakilishi wenye kura (electoral college), ambapo rais huchaguliwa kwa muhula wa miaka minne. Inawezekana pia kwamba rais achaguliwe kupitia katika Nyumba ya Wawakilishi ya Marekani (US House of Representatives), ikiwa kongamano la wajumbe halikuweza kumchagua rais kwa kumpa mgombea mmoa kura nyingi kuliko mwingine yeyote. Kulingana na Katiba ya Marekani, mtu yeyote hawezi kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo zaidi ya mara mbili.[1] Kukitokea kifo, kujiuzulu au kuondelewa mamlakani kwa rais, Makamu wa Rais wa Marekani atachukulia kiti cha rais. Orodha hii inajumulisha tu wale watu ambao waliapishwa kama rais kufuatia kupitishwa ka Katiba ya Marekani hapo 4 Machi 1789.

Ikulu ya White House, makazi rasmi ya rais wa Marekani
Ngao ya Taifa la Marekani.

Kumeapishwa marais 45, na kumekuwa na marais 46, kwa sababu rais Grover Cleveland alihudumu mihula miwili isiyofuatana, na kwa hivi anahesabiwa mara mbili, kama rais nambari 22 na nambari 24. Marais wanne walifariki kawaida wakiwa mamlakani (William Henry Harrison, Zachary Taylor, Warren G. Harding, na Franklin D. Roosevelt), mmoja akajiuzulu (Richard Nixon), na wanne wakauawa (Abraham Lincoln, James A. Garfield, William McKinley, na John F. Kennedy). Rais wa kwanza wa Marekani alikuwa George Washington, aliyeapishwa 1789 bada ya kupigiwa kura na wajumbe wote katika kongamano. William Henry Harrison alihudumu kwa muda wa siku 31 pekee, mwaka 1841, naye Franklin D. Roosevelt akahudumu kwa muda mrefu zaidi kuliko wote, miaka 12. Rais wa sasa ni Joe Biden, aliyeapishwa 20 Januari 2021.

Marais hariri

Urais Jina la Rais Kipindi cha utawala Chama Jimbo la kuzaliwa Makamu wa Rais
1 George Washington   1789 - 1797 Independent Virginia John Adams
2 John Adams   1797 - 1801 Federalist Massachusetts Thomas Jefferson
3 Thomas Jefferson   1801 - 1809 Republican (Jeffersonian) Virginia Aaron Burr | George Clinton
4 James Madison   1809 - 1817 Republican (Jeffersonian) Virginia Elbridge Gerry
5 James Monroe   1817 - 1825 Republican (Jeffersonian) Virginia Daniel Tompkins
6 John Quincy Adams   1825 - 1829 National Republican Massachusetts John Calhoun
7 Andrew Jackson   1829 - 1837 Democratic South Carolina John Calhoun | Martin Van Buren
8 Martin Van Buren   1837 - 1841 Democratic New York Richard Mentor Johnson
9 William Harrison   1841* Whig Virginia John Tyler
10 John Tyler   1841 - 1845 Whig Virginia
11 James Polk   1845 - 1849 Democrat North Carolina George Dallas
12 Zachary Taylor   1849 - 1850* Whig Virginia Millard Fillmore
13 Millard Fillmore   1850 - 1853 Whig New York
14 Franklin Pierce   1853 - 1857 Democrat New Hampshire William King
15 James Buchanan   1857 - 1861 Democrat Pennsylvania John Breckinridge
16 Abraham Lincoln   1861 - 1865* Republican Kentucky Hannibal Hamlin | Andrew Johnson
17 Andrew Johnson   1865 - 1869 Democrat North Carolina
18 Ulysses Grant   1869 - 1877 Republican Ohio Schuyler Colfax | Henry Wilson
19 Rutherford Hayes   1877 - 1881 Republican Ohio William Wheeler
20 James Garfield   1881 - 1881* Republican Ohio Chester Arthur
21 Chester Arthur   1881 - 1885 Republican Vermont
22 Grover Cleveland   1885 - 1889 Democrat New Jersey Thomas Hendricks
23 Benjamin Harrison   1889 - 1893 Republican Ohio Levi Morton
24 Grover Cleveland   1893 - 1897 Democrat New Jersey Adlai Stevenson
25 William McKinley   1897 - 1901* Republican Ohio Garret Hobart | Theodore Roosevelt
26 Theodore Roosevelt   1901 - 1909 Republican New York Charles Fairbanks
27 William Howard Taft   1909 - 1913 Republican Ohio James Sherman
28 Woodrow Wilson   1913 - 1921 Democrat Virginia Thomas Marshall
29 Warren Harding   1921 - 1923* Republican Ohio Calvin Coolidge
30 Calvin Coolidge   1923 - 1929 Republican Vermont Charles Dawes
31 Herbert Hoover   1929 - 1933 Republican Iowa Charles Curtis
32 Franklin Roosevelt   1933 - 1945* Democrat New York John Garner | Henry Wallace | Harry Truman
33 Harry Truman   1945 - 1953 Democrat Missouri Alben Barkley
34 Dwight Eisenhower   1953 - 1961 Republican Texas Richard Nixon
35 John Kennedy   1961 - 1963* Democrat Massachusetts Lyndon Johnson
36 Lyndon Johnson   1963 - 1969 Democrat Texas Hubert Humphrey
37 Richard Nixon   1969 - 1974** Republican California Spiro Agnew | Gerald Ford
38 Gerald Ford   1974 - 1977 Republican Nebraska Nelson Rockefeller
39 Jimmy Carter   1977 - 1981 Democrat Georgia Walter Mondale
40 Ronald Reagan   1981 - 1989 Republican Illinois George H. W. Bush
41 George H. W. Bush 1989 - 1993 Republican Massachusetts Dan Quayle
42 Bill Clinton   1993 - 2001 Democrat Arkansas Al Gore
43 George W. Bush   2001 - 2009 Republican Connecticut Dick Cheney
44 Barack Obama   2009 - 2017 Democrat Hawaii Joe Biden
45 Donald Trump   2017 - 2021 Republican New York Mike Pence
46 Joe Biden   2021 - Democrat Pennsylvania Kamala Harris


'*' maana yake, amefariki madarakani

'**' maana yake, amejiuzulu madarakani

Marejeo hariri

Viungo vya Nje hariri