Michezo ya Afrika Nzima

(Elekezwa kutoka Michezo ya Africa Nzima)

Michezo ya Afrika Nzima (pia huitwa Michezo ya Afrika au Michezo ya Pan Afrika) ni tukio la michezo mbalimbali ya mataifa ya Afrika linalofanyika kila baada ya miaka minne, linaloandaliwa na Muungano wa Kamati za Kitaifa za Olimpiki za Afrika (ANOCA). Mataifa yote yanayoshiriki lazima yawe ya bara la Afrika.

Lagos 1973

Tukio la kwanza lilifanyika mwaka wa 1965 katika mji wa Brazzaville, nchini Jamhuri ya Kongo. Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) ilitoa utambulisho rasmi kwa tukio hilo kama tukio la bara la michezo mbalimbali, sambamba na michezo ya Pan American na Michezo ya Bara la Asia.

Historia

hariri

Mwanzilishi wa Olimpiki ya kisasa Pierre de Coubertin alianzisha michezo ya Pan African mapema mwaka wa 1920. Mamlaka za kikoloni zilizokuwa zinatawala Afrika wakati huo zilikuwa zinahofia wazo hilo, zikishuku kuwa umoja wa Waafrika kwa njia ya mchezo kungesababisha Waafrika kudai uhuru wao.

Majaribio yalifanywa ili kuandaa michezo hiyo Algiers, nchini Algeria, na Alexandria, nchini Misri, miaka 1925 na 1928, lakini licha ya maandalizi kabambe yaliyofanywa na waratibu, juhudi hizo zilitumbukia nyongo. Mwanachama wa kwanza kutoka Afrika wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, mwanariadha wa masafa mafupi aliyezaliwa nchini Ugiriki mwenye uraia wa Misri, Angelo Bolanaki, alichangia fedha kujengwe uwanja, lakini michezo haikufanyika hadi baada ya miongo mingine mitatu.

Katika miaka ya mapema ya 1960, nchi za Afrika zilizokuwa zinazungumza Kifaransa zilipanga Michezo ya Urafiki. Michezo hiyo ilipangwa na Madagascar (1960) na kisha Côte d'Ivoire (1961). Michezo ya tatu ilipangwa kufanyika nchini Senegal mwaka wa 1963.

Kabla ya michezo hiyo kukamilika, Mawaziri wa Vijana na Mchezo wa Kiafrika walikutana Paris mwaka wa 1962, na kwa sababu chache za nchi zilizokuwa zinazungumza Kiingereza zilikuwa tayari zinashiriki, wao wakaipa Michezo hiyo jina la Michezo ya Pan Africa. Michezo hiyo ilipewa utambulisho rasmi na IOC kuwa katika kiwango sawa na michezo mingine ya kibara kama vile michezo ya bara Asia na Michezo ya Pan America.

Mnamo Julai mwaka wa 1965, toleo la kwanza lilifanyika Brazzaville, nchini Congo, sasa ikijulikana kama michezo ya All-Africa. Kutoka mataifa 30, idadi ya wanariadha karibu 2500 walishiriki. Misri ilishikilia nafasi ya kwanza kwa kupata idadi kubwa ya medali.

Katika mwaka wa 1966, Kamati Kuu ya Michezo katika Afrika (SCSA) ilipangwa mjini Bamako; inasimamia michezo ya All-Africa. Toleo la pili lilituzwa nchi ya Mali katika mwaka wa 1969, lakini mapinduzi ya kijeshi yalilazimisha kufutiliwa mbali kwa Michezo hiyo. Lagos, Nigeria ilijitolea kuwa mwenyeji wa michezo hiyo mwaka wa 1971. Hatimaye michezo hiyo ilifanyika mwaka wa 1973 kutokana na Vita vya Biafra, ambavyo vilikuwa vimekwisha karibuni nchini Nigeria.

Katika mwaka wa 1977, toleo la 3 la michezo hiyo lilikuwa limepangwa kufanyika nchini Algeria, lakini kutokana na sababu za kiufundi, yaliahirishwa kwa muda wa mwaka moja na yalifanyika mwaka wa 1978.

Kwa kuendeleza mtindo huo, toleo lililofuata lilipangwa kufanyika nchini Kenya mwaka wa 1983, lakini lilisogezwa hadi mwaka wa 1985 na hatimaye yalifanyika mjini Nairobi mwaka wa 1987.

Mtindo wa Olimpiki wa miaka minne haujakosa kufuatwa, na michezo hiyo imepangwa Cairo, Harare, Johannesburg, na Lagos. Katika mwaka wa 2007, Algiers kwa mara nyingine tena ilikuwa mwenyeji wa michezo na kuwa ya kwanza kurudia uenyeji wa michezo hii. Lusaka nchini Zambia imejiondoa (mnamo Desemba 2008) kama mwenyeji wa toleo lijalo la michezo hiyo mwaka wa 2011.

Miji wenyeji wa michezo hii

hariri
Orodha Mwaka Jiji Nchi Tarehe Nchi yenye medali nyingi
1 1965 Brazzaville   Congo-Brazzaville 18 Julai - 25 Julai 1965   United Arab Republic
-- 1969 Bamako   Mali Ulikatizwa kutokana na mapinduzi ya kijeshi
2 1973 Lagos   Nigeria 7 Januari - 18 Januari 1973   Egypt
3 1978 Algiers   Algeria 13 Julai - 28 Julai 1978   Tunisia
4 1987 Nairobi   Kenya 1 Agosti - 12 Agosti 1987   Egypt
5 1991 Cairo   Egypt 20 Septemba - 1 Oktoba 1991   Egypt
6 1995 Harare   Zimbabwe 13 Septemba - 23 Septemba 1995   South Africa
7 1999 Johannesburg   South Africa 10 Septemba - 19 Septemba 1999   South Africa
8 2003 Abuja   Nigeria 5 Oktoba - 17 Oktoba 2003   Nigeria
9 2007 Algiers   Algeria 11 Julai - 23 Julai 2007   Egypt
10 2011 Maputo   Mozambique 15 Julai - 27 Julai 2011

Mji utakaokuwa mwenyeji wa makala ya 2015 ya michezo hii utaamuliwa hivi karibuni. Accra, Ghana na Kenya zimetajwa kama zenye uwezekano wa kuwa wenyeji.

Orodha ya medali

hariri

Orodha inayofuata inaonyesha medali zilizohesabiwa katika matukio yote ya michezo hii.

Nafasi Nchi Dhahabu Fedha Shaba -Jumla Mwaka wa
medali ya kwanza
1   Misri 431 328 320 1079 1965
2   Nigeria 303 277 256 836 1965
3   Afrika Kusini 198 174 137 509 1995
4   Algeria 132 152 189 473 1965
5   Tunisia 123 [85] 133 362 1965
6   Kenya 90 97 104 291 1965
7   Senegal 40 40 73 153 1965
8   Ghana 26 38 64 128 1965
9   Ethiopia 23 29 34 86 1965
10   Cameroon 20 42 81 143 1965
11   Zimbabwe 18 26 57 101 1987
12   Uganda 17 19 33 69 1965
13   Côte d'Ivoire 17 18 33 68 1965
14   Madagascar 10 15 33 58 1965
15   Moroko 9 12 15 36 1973
16   Angola 9 7 17 33 1987
17   Lesotho 8 3 8 19 1991
18   Mauritius 6 19 27 52 1987
19   Libya 6 8 16 30 1978
20   Namibia 4 10 15 29 1991
21   Tanzania 4 8 10 22 1965
22   Zambia 4 4 22 30 1965
23   Mali 4 4 7 16 1965
24   Gabon 4 4 19 27 1965
25   Botswana 4 4 10 18 1991
26   Mozambique 4 2 [1] 7 1987
27   Eritrea 3 [1] 2 6 2007
28   Sudan 3 [1] 3 7 1973
29   Democratic Republic of the Congo 2 3 6 11 1965
30   Republic of the Congo [1] 7 15 23 1965
31   Central African Republic [1] 2 2 5 1991
32   Guinea [1] 2 [1] 4 1973
  Sierra Leone [1] 2 [1] 4 1991
33   Eswatini [1] 0 9 10 1973
34   Chad [1] 0 9 10 1965
35   Cape Verde [1] 0 2 3 1999
36   Burkina Faso [1] 0 [1] 2 1987
37   Somalia [1] 0 0 [1] 1973
38   Seychelles 0 13 18 31 1987
39   Burkina Faso 0 3 7 10 1965
40   Togo 0 2 10 12 1965
41   Niger 0 2 6 8 1965
42   Benin 0 2 3 5 1973
43   Gambia 0 2 0 2 1973
44   Rwanda 0 2 0 2 1987
45   São Tomé and Príncipe 0 [1] [1] 2 2003
46   Malawi 0 0 2 2 1987
47   Guinea-Bissau 0 0 [1] [1] 1999

Ushawishi

hariri

Baada ya kusikia kuhusu michezo ya Pan-Afrika wakati akiwa katika ziara za kibiashara huko Kongo, mwanadiplomasia Mrusi - Muarmenia Ashot Melik-Shahnazaryan alipata wazo la kuanzisha michezo ya Pan-Armenia.

Angalia Pia

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri