Uislamu katika Jamhuri ya Kongo

Uislamu kwa nchi

Uislamu katika eneo la Jamhuri ya Kongo ulifika katika karne ya 19 wakati wafanyabiashara kutoka Afrika ya Mashariki walifika kwa biashara ya pembe za ndovu na ya watumwa. [1]

Kuna makadirio tofauti kuhusu idadi ya Waislamu nchini kati ya asilimia 1.5 hadi 10.[2][3]

Mnamo mwaka wa 2005 msikiti mpya mkubwa ulijengwa mjini Brazzaville. Ni kwamba wafanyakazi wengi wa mijini ni wahamiaji kutoka Afrika ya Magharibi na Lebanon, na baadhi kutoka Afrika ya Kaskazini. Wahamiaji kutoka Afrika Magharibi hasa ni kutoka Mali, Benin, Togo, Mauritania na Senegal. Walebanoni wengi ni Sunni. Pia kulikuwa na kundi kubwa la Waislamu kutoka Chad.

Waislamu walio wengi ni Wasunni wa madhhab ya Maliki, wachache Washia au Waahmadiyya.

Siku tukufu za Kiislamu hazitajwi kitaifa; lakini, zinaheshimiwa. Waajiri wanawakubalia likizo wale ambao wanataka kupumzika na sikukuu zao hazimo katika kalenda ya taifa.[4]

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. www.cp-pc.ca
  2. "CIA factbook intaja 10% Waislamu". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-12-24. Iliwekwa mnamo 2015-05-10.
  3. Pewforum inataja 1.5% Waislamu
  4. www.state.gov