Jimbo Katoliki la Sumbawanga
Jimbo Katoliki la Sumbawanga (kwa Kilatini "Dioecesis Sumbavangensis") ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania, na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Kanisa kuu liko mjini Sumbawanga, katika mkoa wa Rukwa.
Lilianzishwa tarehe 10 Mei 1946 na linahusiana na Jimbo Kuu la Mbeya.
Askofu wa sasa ni Beatus Christian Urassa, ALCP/OSS.
Takwimu
haririEneo lake lote ni kama kilometa mraba 28.654, ambamo wamo wakazi 1,244,330. Kati yao Wakatoliki ni 757,451 (2014) yaani asilimia 60.9.
Waamini hawa wanahudumiwa na mapadri 48, ambao kati yao 42 ni wanajimbo na 6 watawa. Hivyo kwa wastani kila mmojawao anahudumia waamini 15,780.
Parokia ziko 24.
Mlolongo wa maaskofu
hariri- James Holmes-Siedle, M.Afr. (29 Julai 1946 - 5 Agosti 1958 kuhamishiwa Jimbo Katoliki la Kigoma)
- Charles Msakila (13 Novemba 1958 - 23 Februari 1994 kufariki dunia)
- Damian Kyaruzi (21 Aprili 1997 - 19 Aprili 2018 kustaafu)
- Beatus Christian Urassa, ALCP/OSS (tangu 19 Aprili 2018)
Viungo vya nje
hariri- Giga-Catholic Information
- Catholic Hierarchy
- [1] Archived 26 Mei 2015 at the Wayback Machine. katika tovuti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
- Bolla Quo maiora, AAS 39 (1947), uk. 80
- Bolla Quemadmodum ad Nos, AAS 45 (1953), uk. 705
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Sumbawanga kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |