15 Agosti
tarehe
(Elekezwa kutoka Agosti 15)
Jul - Agosti - Sep | ||||||
1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 |
8 | 9 | 10 | 11 | 12 | 13 | 14 |
15 | 16 | 17 | 18 | 19 | 20 | 21 |
22 | 23 | 24 | 25 | 26 | 27 | 28 |
29 | 30 | 31 | ||||
Kalenda ya Gregori |
Tarehe 15 Agosti ni siku ya 227 ya mwaka (ya 228 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 138.
Matukio
hariri- 1537 - Mji wa "Nuestra Señora Santa María de la Asunción" unaundwa kando ya mto Paraguay: utakuwa mji mkuu wa nchi ya Paraguay
- 1888 - Shirika la Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki linaanza kutawala pwani ya Tanganyika iliyokodiwa na Zanzibar - chanzo cha vita ya Abushiri
- 1945 - Japani inajisalimisha; mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia katika Asia
- 1960 - Jamhuri ya Kongo inapata uhuru kutoka Ufaransa
- 1971 - Nchi ya Bahrain inapata uhuru kutoka Uingereza
Waliozaliwa
hariri- 1195 - Mtakatifu Antoni wa Padua, padri wa shirika la Ndugu Wadogo na mwalimu wa Kanisa kutoka Ureno
- 1607 - Mtakatifu Fransisko Ferdinando de Capillas, O.P., padri kutoka Hispania aliyekuwa wa kwanza kufia dini ya Ukristo nchini China
- 1654 - Mtakatifu Yohane Yosefu wa Msalaba, O.F.M., padre kutoka Italia
- 1769 - Napoleon Bonaparte, Kaisari wa Ufaransa
- 1885 - Edna Ferber, mwandishi kutoka Marekani
- 1897 - Louis-Victor Broglie, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia, mwaka wa 1929
- 1923 - Rose Marie, mwigizaji wa filamu kutoka Marekani
- 1925 - Oscar Peterson, mwanamuziki wa Kanada
- 1930 - Tom Mboya, mwanasiasa wa Kenya
- 1931 - Richard Heck, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia, mwaka wa 2010
- 1943 - Barbara Bouchet, mwigizaji filamu wa Italia
- 1956 - Daniel Nicodemus Nsanzugwako, mwanasiasa wa Tanzania
- 1974 - Natasha Henstridge, mwigizaji wa filamu kutoka Kanada
Waliofariki
hariri- 423 - Honorius, Kaisari wa Dola la Roma Magharibi (tangu 395)
- 465 - Libius Severus, Kaisari wa Dola la Roma Magharibi
- 1038 - Mtakatifu Stefano wa Hungaria, mfalme aliyeingiza taifa lake katika Ukristo wa Kanisa Katoliki
- 1936 - Grazia Deledda, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 1926
- 1982 - Hugo Theorell, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 1955
- 2004 - Sune Bergström, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 1982
Sikukuu
haririWakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha sherehe ya Bikira Maria Kupalizwa mbinguni (Waorthodoksi wanaiita Kulala kwa Mama wa Mungu), lakini pia kumbukumbu za watakatifu Tarsisi wa Roma, Stratoni na wenzake, Simplisiani, Alipius wa Thagaste, Altifridi, Yasinto wa Krakau, Stanislaus Kostka, Alois Batis na wenzake n.k.
Viungo vya nje
hariri- BBC: On This Day
- On This Day in Canada Archived 2012-12-09 at Archive.today
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu 15 Agosti kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |