Jimbo Katoliki la Same
Jimbo Katoliki la Same (kwa Kilatini "Dioecesis Samensis") ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania, na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Kanisa kuu liko mjini Same, katika mkoa wa Kilimanjaro na limewekwa wakfu kwa heshima ya Kristo Mfalme.
Linahusiana na Jimbo Kuu la Arusha.
Takwimu
haririEneo lake lote ni kama kilometa mraba 10,000, ambamo wamo wakazi 562,950. Kati yao Wakatoliki ni 70,490 (2004) yaani asilimia 12.5.
Waamini hawa wanahudumiwa na mapadri 85, ambao kati yao 74 ni wanajimbo na 9 watawa. Parokia ziko 30, Parokia Teule 5.
Historia
hariri- 10 Desemba 1963: Kuanzishwa kwa Apostolic Prefecture ya Same kutokana na Jimbo Katoliki la Moshi
- 3 Februari 1977: Kufanywa jimbo kamili
Uongozi
hariri- Apostolic Prefect
- Maaskofu
- Josaphat Louis Lebulu (12 Februari 1979 - 28 Novemba 1998 kufanywa askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha)
- Jacob Venance Koda (16 Machi 1999 - 15 Aprili 2010 kujiuzulu)
- Rogatus Kimaryo, C.S.Sp. (30 Aprili 2010 - )
Viungo vya nje
hariri- Giga-Catholic Information
- Catholic Hierarchy
- Hati Adpetens Natalis Christi
- Hati Praefecturam illam, AAS 69 (1977), uk. 318
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Same kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |