Jimbo Kuu la Arusha
Jimbo Kuu la Arusha (kwa Kilatini "Archidioecesis Arushaënsis") ni mojawapo kati ya majimbo 34 (2012) ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Chini yake kuna kanda ya Kanisa yenye majimbo yafuatayo: Moshi, Same na Mbulu.
Askofu mkuu wake ni Isaac Amani Massawe.
Kanisa kuu liko mjini Arusha na limewekwa wakfu kwa heshima ya Mt. Teresa.
Historia
hariri- 1 Machi 1887: Kuanzishwa na Papa Yohane XXIII kama jimbo kutokana na Jimbo Katoliki la Moshi
- 16 Machi 1999: Kupandishwa cheo kuwa jimbo kuu
Uongozi
hariri- Askofu Mkuu
- Isaac Amani Massawe (tangu 2018)
- Josaphat Louis Lebulu (28 Novemba 1998 - 2018)
- Maaskofu
Takwimu
haririEneo la jimbo kuu lina kilometa mraba 67,340, yaani mkoa wa Arusha na sehemu ya mkoa wa Manyara.
Kati ya wakazi 1,705,687 (2004) Wakatoliki ni 193,446 (sawa na 11.3%) katika parokia 30.
Mapadri ni 86 (42 wanajimbo na 44 watawa), hivyo kwa wastani kila mmojawao anahudumia waumini 2,249.
Viungo vya nje
hariri- Catholic Hierarchy
- Giga Catholic
- Tovuti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
- Hati Christi mandata Archived 20 Desemba 2011 at the Wayback Machine., AAS 56 (1964), uk. 247
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Kuu la Arusha kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |