Jamhuri ya Kongo

nchi ya Afrika ya Kati
(Elekezwa kutoka Kongo (Jamhuri ya))


Jamhuri ya Kongo ni nchi ya Afrika ya Kati. Imejulikana pia kama Kongo-Brazzaville (kutokana na mji mkuu) kwa kusudi la kutoichanganywa na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Jamhuri ya Kongo

Jamhuri ya Kongo imepakana na Gabon, Kamerun, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Angola na Bahari ya Atlantiki.

Nchi ilikuwa koloni la Ufaransa hadi tarehe 15 Agosti 1960.

Historia hariri

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani na ya Wabilikimo.

Katika karne za BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi waliotawala eneo lote na kuendesha biashara katika beseni ya mto Kongo.

Baadaye eneo hilo lilikuwa sehemu ya koloni la Afrika ya Kiikweta ya Kifaransa

Baada ya uhuru tarehe 15 Agosti 1960 nchi ilitawaliwa na Wakomunisti tangu mwaka 1970 hadi 1991.

Kuanzia mwaka 1992 zilifanyika chaguzi kwa mfumo wa vyama vingi, lakini mwaka 1997 vilitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Rais Denis Sassou Nguesso ametawala miaka 36 kati ya 41 ya mwisho.

Watu hariri

Sehemu kubwa ya nchi ni misitu, hivyo wakazi wengi (70%) wanaishi mijini upande wa kusini-magharibi wa nchi. Kati yao, 48% ni wa kabila la Wakongo, 20% Wasangha, 17% Wateke, 12% Wam'Bochi. 2% ni Wabilikimo.

Nchi ina lugha 62 tofauti, zikiwemo lugha 2 za taifa: Kingala na Kikongo (Kituba). Hata hivyo lugha rasmi ni Kifaransa.

Wakazi wengi ni Wakristo (87.1%), wakiwemo Waprotestanti (51.4%) na Wakatoliki (33.1%), ingawa asilimia zinazotajwa hazilingani. Waislamu ni 1.2%, wafuasi wa dini asilia za Kiafrika ni 2.7% na wa Baha'i 0.4%.

 
Ramani ya Mikoa ya Jamhuri ya Kongo

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Serikali
Taarifa za jumla
Utalii


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Kongo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.