Visiwa vya Kanari

(Elekezwa kutoka Canarias)
Comunidad Autonoma de
Canarias
Jimbo la Kujitawala la Visiwa vya Kanari
Miji Mikuu Santa Cruz de Tenerife
Las Palmas de Gran Canaria
Eneo


 - jumla
 - % za Hispania



7.447 km²
1,5%

Wakazi


 - jumla (2011)
 - % za Hispania
 - Msongamano wa watu



2,117,519
4,4%
280 ab./km²

Uwakilishi bungeni


 Nafasi za bunge la wananchi (Congresso)
 Nafasi kwenye bunge la majimbo (Senato)

 

14
2

Rais wa serikali ya Kanari Adán Martín Menis (CC)
Tovuti rasmi Gobierno de Canarias

Visiwa vya Kanari (kwa Kihispania: Islas Canarias) ni funguvisiwa la Afrika ya Kaskazini katika bahari ya Atlantiki. Viko baharini km 150 magharibi kwa Moroko. Umbali na Hispania ni masaa mawili kwa ndege.

Visiwa vya Kanari na Hispania

Visiwa vikubwa ni saba:

El Hierro, La Gomera, La Palma na Tenerife ambavyo vinaunda mkoa wa Santa Cruz de Tenerife,

halafu Gran Canaria, Fuerteventura na Lanzarote ambavyo vinaunda mkoa wa Las Palmas,

tena kuna visiwa vidogo sita vya Alegranza, Kisiwa cha Lobos, La Graciosa, Montaña Clara, Roque del Este na Roque del Oeste, vyote vya mkoa wa Las Palmas.

Utawala

hariri

Kisiasa visiwa hivyo ni kati ya maeneo ya kujitawala ndani ya ufalme wa Hispania.

Miji mikubwa ni Las Palmas de Gran Canaria (wakazi 378.628), Santa Cruz de Tenerife (wakazi 221.567), San Cristóbal de la Laguna (wakazi 141.627), Telde (wakazi 96.547) na Arona (79.377).

Miji mikuu ni Santa Cruz de Tenerife na Las Palmas de Gran Canaria. Makao ya mkuu wa serikali ya eneo huhamahama kati ya miji hiyo miwili kila baada ya miaka minne.

Wakazi

hariri

Jumla ya wakazi, kufuatana na sensa ya mwaka 2005 ni 1,968,280. Mkoa wa Las Palmas una wakazi 1.011.928 katika tarafa 33, mkoa wa Santa Cruz de Tenerife una watu 956.352 katika tarafa 52.

 
Ramani ya Visiwa vya Kanari

Idadi ya wakazi wa visiwa vikubwa ni kama ifuatayo:

  • Tenerife - 906.854
  • Gran Canaria - 802.247
  • Lanzarote - 123.039
  • Fuerteventura - 86.642
  • La Palma - 85.252
  • La Gomera - 21.746
  • El Hierro - 10.477

Karibu wenyeji wote ni Wakristo wa Kanisa Katoliki.

Historia

hariri

Visiwa vya Kanari vilitembelewa zamani na wasafiri Wafinisia, Wagiriki na Waroma, baadaye na Waarabu. Katika Ulaya visiwa vilisahauliwa hadi mwaka 1400 hivi.

Visiwa vilikaliwa na wazawa walioitwa Guancha na Wahispania walipofika Kanari. Hakuna uhakika kuhusu asili yao. Wataalamu wengi hufikiri walikuwa Waberber. Wengine husema walikuwa wafungwa walioachiwa huru visiwani wakati wa Dola la Roma.

Wakati wa kufika kwa Wahispania kuanzia mwaka 1400 walikuwa na utamaduni bila chuma; wanasemekana hawakujua usafiri wa bahari.

Katika muda wa karne moja Wahispania walivamia visiwa na kukandamiza utamaduni wa wenyeji. Lugha yao imekwisha kabisa ingawa kuna bado majina ya mahali visiwani kutokana na lugha ya Kiguancha.

Baada ya Wahispania kufika Amerika, Las Palmas ilikuwa bandari muhimu ya safari za Atlantiki.

Uchumi

hariri

Kutokana na uzuri wa nchi na hali ya hewa ambayo ni poa mwaka wote utalii umekuwa nguzo ya uchumi wa visiwa vya Kanari pamoja na kilimo cha mazao ya biashara yanayopelekwa Ulaya, hasa ndizi na tumbaku.


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Kanari kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.