Kanisa Katoliki la Kibizanti nchini Italia
Kanisa Katoliki la Kibizanti nchini Italia ni mojawapo kati ya madhehebu ya Ukristo wa mashariki yenye ushirika kamili na Papa na Kanisa Katoliki lote.
Linafuata mapokeo ya Ukristo wa Ugiriki na kutumia liturujia ya Ugiriki.
Tangu mwanzo wa Kanisa katika rasi ya Italia kulikuwa na Wakristo waliotumia lugha ya Kigiriki, hata mjini Roma, lakini hasa katika maeneo ya kusini.
Baada ya kutokea Ukristo wa mashariki na Ukristo wa magharibi, maeneo hayo yalishindaniwa.
Wakristo wa mashariki nchini Italia waliongezeka hasa baada ya Albania kuvamiwa na Waturuki Waislamu. Hapo Waalbania wengi walivuka bahari na kukimbilia usalama hasa katika Ufalme wa Sicilia.
Ingawa wengi walimezwa na mazingira mapya, wengine walidumisha lugha yao ya Kialbania pamoja na madhehebu ya Kigiriki.
Hatimaye walipewa na Papa uongozi kamili (6 Februari 1784) na hatimaye (1919) walianzishiwa majimbo mawili, mbali na monasteri huru ya Grottaferrata.
Mwaka 2010, waamini wa Kanisa hilo walikadiriwa kuwa 61,000 hivi katika parokia 45, chini ya maaskofu 2, mapadri 82 (baadhi wakiwa na ndoa) na mashemasi 5. Pia kulikuwa na watawa wasio na daraja takatifu 207.[1]
Tanbihi
hariri- ↑ Ronald Roberson. "The Eastern Catholic Churches 2010" (PDF). Catholic Near East Welfare Association. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-09-23. Iliwekwa mnamo December 2010.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
(help) Information sourced from Annuario Pontificio 2010 edition
Marejeo
hariri- Oriente Cattolico (Vatican City: The Sacred Congregation for the Eastern Churches, 1974)
- Annuario Pontificio
- "Italo-Greeks". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913. http://en.wikisource.org/wiki/Catholic_Encyclopedia_(1913)/Italo-Greeks.
- Fortescue, Adrian. The Uniate Eastern Churches: the Byzantine Rite in Italy, Sicily, Syria and Egypt. Ed. George D. Smith. New York: F. Ungar, 1923. Print.
Viungo vya nje
hariri- Hati Orientalium Ecclesiarum ya Mtaguso wa pili wa Vatikano
- Hati Orientales omnes Ecclesias ya Papa Pius XII
- [1] Ilihifadhiwa 5 Machi 2012 kwenye Wayback Machine. - Hati ya Papa Yohane Paulo II Orientale Lumen kuhusu Makanisa ya Mashariki
- Codex Canonum Ecclesiarum Orientalium Ilihifadhiwa 5 Machi 2012 kwenye Wayback Machine. - Mkusanyo wa Sheria za Makanisa ya Mashariki (katika Kilatini pamoja na sehemu sambamba)
- Instruction for Applying the Liturgical Prescriptions of the Code of Canons of the Eastern Churches Ilihifadhiwa 25 Aprili 2009 kwenye Wayback Machine. - Hati ya Idara ya Papa kwa Makanisa ya Mashariki kuhusu liturujia
- Ujuzi wa msingi kuhusu Makanisa hayo Ilihifadhiwa 17 Mei 2011 kwenye Wayback Machine.
- CNEWA Idara ya Papa inayosaidia Makanisa hayo Ilihifadhiwa 9 Machi 2009 kwenye Wayback Machine.
- Sura ya Idara ya Papa kwa Makanisa hayo
- Takwimu za Makanisa hayo Ilihifadhiwa 27 Juni 2007 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kanisa Katoliki la Kibizanti nchini Italia kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |