Palestina
Palestina (kwa Kiarabu: فلسطين filasṭīn, falasṭīn; kutoka Kilatini: Palaestina; kwa Kiebrania: פלשתינה Palestina) ni jina la eneo lililoko upande wa Mashariki wa Bahari ya Mediteranea kati ya mkingo wa bahari hiyo na mto Yordani.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: Biladi | |||||
Mji mkuu | Ramallah na Gaza hali halisi kama makao ya ofisi za serikali. Yerusalemu ya Mashariki ni mji mkuu wa Palestina unaotazamiwa. | ||||
Mji mkubwa nchini | Gaza | ||||
Lugha rasmi | Kiarabu | ||||
Serikali | Mahmoud Abbas Rami Hamdallah | ||||
Katiba Uhuru ilitangazwa Hali |
15 Novemba 1988 Haitambuliwi | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
6,220 km² (ya 169) 3.54 | ||||
Idadi ya watu - 2015 kadirio - Msongamano wa watu |
4,682,467 (ya 123) 595/km² (ya 18) | ||||
Fedha | Shekel ya Israel Dinari ya Yordania ( JOD, ILS )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+2) (UTC+3) | ||||
Intaneti TLD | .ps | ||||
Kodi ya simu | +970b
- | ||||
a West Bank pekee. b si rasmi. |
Historia ya jina na eneo la Palestina hadi 1948
Asili ya jina ilikuwa nchi ya Wafilisti iliyokuwa kanda nyembamba ya ardhi karibu na pwani ya bahari. Waroma wa kale walitumia jina hilo kwa jumla ya jimbo lao katika sehemu hizi.
Baada ya uvamizi wa Waarabu Waislamu jina liliendelea kutumiwa kwa umbo la Kiarabu "Filastin" na kutazamwa kama sehemu ya Shamu au Syria.
Tangu mwaka 1516 eneo lilitawaliwa na Milki ya Osmani. Kwa muda mrefu maeneo ya Palestina yalikuwa sehemu ya kusini ya jimbo la Dameski, na katika karne ya 19 jimbo la pekee la Yerusalemu liliundwa.
Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Uingereza ulitawala eneo hili kama eneo la kukabidhiwa la Shirikisho la Mataifa, na eneo hili lilikuwa pamoja na sehemu kubwa upande wa mashariki wa mto Yordani. Waingereza waligawa eneo katika sehemu mbili upande wa magharibi (Palestina yenyewe) na upande wa mashariki wa mto Yordani uliokuwa baadaye milki ya Yordani.
Kwenye sehemu ya magharibi iliyokuwa Palestina yenyewe kulikuwa na uhamiaji wa Wayahudi kutoka nchi za Ulaya ulioweka msingi kwa mapambano kati ya Israeli na Palestina ya baadaye.
Mwaka 1947 Umoja wa Mataifa uliamua kugawa Palestina katika sehemu tatu zilizopangwa kama Dola la Kiyahudi, Dola la Kiarabu na Yerusalemu kama mji wa kimataifa. Lakini Wayahudi walitangaza uhuru wa Dola la Israeli. Wenyeji Waarabu walipinga azimio hili na vita ilitokea. Baada ya mkataba wa kusalimisha amri Israeli mpya ilikuwa na sehemu ya Palestina kubwa kuliko awali. Asilimia kubwa ya wakazi Waarabu wa sehemu zilizokuwa chini ya Israeli mpya walikimbia au walifukuzwa nje. Ukanda wa Gaza ulishikwa na Misri na Ukingo wa Magharibi wa Yordani ulitawaliwa na milki ya Yordani.
Mapigano ya Wapalestina
Kati ya wakimbizi Waarabu waliokaa katika makambi huko Lebanoni, Syria, Yordani na Gaza kulikuwa na harakati ya kujielewa kama taifa la Wapalestina wakaunda vyama mbalimbali vya kupigania kurudi kwao lakini hii ilishindikana. Baada ya Vita ya siku 6 mwaka 1967 Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Yordani zilitwaliwa na jeshi la Israeli.
Harakati ya Wapalestina Waarabu iliendelea kupigania uhuru. Mapigano haya yalipata namna ya usuluhisho kwa muda na katika mapatano ya Oslo mwaka 1993 yalianzishwa Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina yaliyotangaza Dola la Palestina.
Palestina mpya
Kwa sasa Palestina ni nchi katika mwendo wa kupata uhuru kamili lakini hakuna uhakika mwendo huu utakamilishwa lini.
Maeneo ya Palestina yanatengwa kati ya sehemu chini ya serikali ya Palestina na maeneo yanayosimamiwa na Israeli.
Maeneo haya yako kati ya mto Yordani na pwani ya Mediteranea: ni hasa Ukingo wa Magharibi wa Yordani na Ukanda wa Gaza.
Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina ina kiwango fulani cha madaraka ya kiserikali katika baadhi ya maeneo haya.
Mamlaka hayo hutambuliwa na nchi nyingi za Waarabu kama serikali halisi. Jumuia ya kimataifa kwa ujumla imetambua mamlaka kwa viwango mbalimbali lakini si kama serikali kamili ya nchi huru. Hivyo Mamlaka ina kiti cha mtazamaji kwenye Umoja wa Mataifa.
Maeneo ya Palestina ya sasa yamepakana na Israel, Yordani na Misri. Kanda la Gaza lina pwani kwenye Mediteranea.
Ramani za mabadiliko ya mipaka ya Palestina
-
1 Mapendekezo ya 1916-22 : Mapendekezo matatu kwa utawala wa Palestina baada ya Vita Kuu ya Kwanza. Mstari mwekundi ni mpaka wa "International Administration" iliyopendekezwa katika Mapatano ya Sykes–Picot ya 1916, mstari buluu uliokatwa ni pendekezo la 1919 la Shirika la Uzayuni kwenye Mkutano wa Paris 1919, Na mstari buluu mwembamba ni mipaka ya eneo la kukabidhiwa la Palestina chini ya mamlaka ya Uingereza 1923-48
-
2 Ardhi ya Kiyahudi 1947 : Ardhi iliyokuwa mali ya Wayahudi katika Eneo la kukabidhiwa la Palestina mnamo mwaka 1947. Idadi ya wakazi Wayahudi iliongezeka kuanzia watu 83,790 mwaka 1922 hadi 608,000 mwaka 1946.
-
3Mpango wa Umoja wa Kimataifa kwa Ugawaji wa Palestina 1947 : Azimio la UM lilitaka kugawa Palestina kwa sehemu tatu: Dola la Kiyahudi (nyeupe), Dola la Kiarabu (Kijani) na Yerusalemu kama mji wa pekee.
-
4 1948-67 : Baada ya vita ya uhuru wa Israel Ukanda wa Gaza ulibaki chini ya Misri na Ukingo wa Magharibi ya Yordani chini ya milki ya Yordani. Yerusalemu iligawiwa kati ya Israel na Yordani.
-
5 1993 hadi sasa: Maeneo yaliyo chini ya Serikali ya Palestina.
Tazama pia
Viungo vya nje
- Palestinian Media Watch – Timing and methods of the base of the Palestinian Authority
- The Palestinian Basic Law – A collection of various propsals and amendments to the Basic Law of Palestine
- Columbia University Libraries – Palestine, directory category of the WWW-VL.
- Palestinian Territory Government katika Open Directory Project
Serikali
- State Information Service Archived 11 Agosti 2003 at the Wayback Machine.
- Ministry of Planning Archived 11 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.
- Ministry of Information Archived 2009-04-08 at Archive.today
- (Kiarabu) Ministry of Education and Higher Education Archived 31 Oktoba 2015 at the Wayback Machine.
- Ministry of Education and Higher Education Archived 11 Mei 2008 at the Wayback Machine.
- Ministry of Labor (archive)
- (Kiarabu) The Palestinian Legislative Council Archived 3 Machi 2016 at the Wayback Machine.
- Ministry of the National Economy Archived 18 Oktoba 2015 at the Wayback Machine.
- Negotiations Affairs Department Archived 3 Februari 2020 at the Wayback Machine.
- PECDAR – Palestinian Economic Council for Development and Reconstruction Archived 11 Desemba 2007 at the Wayback Machine.
- Palestine Media Center(Kiarabu)
Israeli na Mamlaka ya Palestina
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Palestina kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |