Arusha (mji)

Jiji kuu la Mkoa wa Arusha, Tanzania
(Elekezwa kutoka Wilaya ya Arusha Mjini)


Arusha ni jiji lililomo kaskazini mwa Tanzania na makao makuu ya Mkoa wa Arusha. Kiutawala eneo la jiji la Arusha ni sawa na eneo la Wilaya ya Arusha Mjini. Ina postikodi namba 23100.

Jiji la Arusha
Mji wa Arusha na Mlima Meru
Mji wa Arusha na Mlima Meru
Mji wa Arusha na Mlima Meru
Mahali paJiji la Arusha
Mahali paJiji la Arusha
Jiji la Arusha is located in Tanzania
Jiji la Arusha
Jiji la Arusha
Majiranukta: 03°22′S 36°41′E / 3.367°S 36.683°E / -3.367; 36.683
Nchi Tanzania
Mkoa Arusha
Wilaya Arusha
Kata 25
Mitaa 155
Serikali[1]
 - Aina ya serikali Halmashauri ya Jiji
 - Mstahiki Meya Maximilian Matle Iranqe
 - Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Hargeney Reginald Chitukuro
Eneo
 - Jumla 267 km²
Mwinuko 1,457 m (4,777 ft)
Idadi ya wakazi (2022)https://www.nbs.go.tz
 - Wakazi kwa ujumla 617,631
 - Mtawanyiko wa watu 1,560/km² (4,040.4/sq mi)
EAT (UTC+3)
Msimbo wa posta 231xx
Kodi ya simu 027
Tovuti:  Halmashauri ya Jiji la Arusha

Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 416,442.[2]: 26  Mwaka 2022 walihesabiwa 617,631 [3].

Mji huo upo kando ya Mlima Meru kwenye ncha ya mashariki mwa Bonde la Ufa na umezungukwa na baadhi ya mandhari maarufu barani Afrika zikiwa pamoja na mbuga za wanyama. Hifadhi ya Arusha, Hifadhi ya Wanyama ya Serengeti na Ngorongoro, Ziwa Manyara, Olduvai Gorge, Hifadhi ya Tarangire na mlima Kilimanjaro vipo karibu na mji huu.

Mji huu umezungukwa na milima kaskazini na mashariki, na mazingira yake ni mchanganyiko wa misitu ya savanna na misitu mabaki. Hali ya hewa ni nzuri sana.

Hadi sasa ni makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na za Mataifa.

Jiografia na hali ya hewa

Licha ya kuwa karibu na ikweta, mwinuko wa Arusha wa mita 1400 kusini mwa Mlima Meru hufanya hali ya hewa yenye ubaridi na unyevu mwingi. Viwango vya joto ni kati ya daraja 13 na 30 na daraja 25 kwa wastani. Ina nyakati tofauti za mvua na ukame na huwa inakumbwa na upepo wa msimu unaovuma toka Bahari Hindi.

Dini ya wakazi wa Arusha ni Ukristo wa madhehebu mbalimbali, kama vile Wakatoliki, Waanglikana, halafu Waislamu na Wahindu.

Historia ya kisiasa

Hati rasmi za uhuru wa Tanzania zilitiwa sahihi hapa na Uingereza mwaka 1961.

Azimio la Arusha la kujitegemea lilipitishwa mjini hapa karibu na maeneo ya mnara wa saa.

Makubaliano ya Arusha ya kusitisha vita nchini Rwanda yalipitishwa mjini Arusha mwaka 1993. Kuanzia 1994 hadi 2015 mjı huu ulikuwa makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda.

Viwanda na Uchumi

Sekta ya msingi ya Mkoa wa Arusha ni kilimo, wazalishaji wa maua na mboga hutuma mazao yao ya hali ya juu Ulaya. Wakulima wadogo wadogo wa kahawa waliathiriwa vibaya na mgogoro wa kahawa wa miaka ya karibuni.

Arusha ina viwanda kadhaa kwa mfano viwanda vya tairi, mimea na madawa.

Mkoa wa Arusha ni chanzo pekee cha madini ya Tanzanite duniani, madini haya yanachimbwa kwa wingi sana na kampuni za madini.

Utalii pia unachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa Arusha. Utalii unachukua nafasi ya pili kwa mchango wa mapato Tanzania. Kutokana na eneo la mji kuwa karibu na vivutio maarufu kama vile Mlima Kilimanjaro, Serengeti na Ngorongoro, Arusha imekuwa maarufu kwa watalii wanaotembelea Tanzania.

 
Mnara wa Uhuru jijini Arusha

Wilaya

 
Kanisa kuu la Arusha
 
Mnara wa Saa wa Arusha

Miongoni mwa maeneo maarufu ya Arusha ni Eneo la biashara, Sekei ambayo ipo Kaskazini-Magharibi, Njiro, kitongoji kinachokua haraka Kusini mwa mji na Soko la Tengeru.

Kaskazini mwa Arusha ziko wilaya za Karatu, Ngorongoro, Monduli, Arusha Vijijini na Longido ambayo ipo kando ya barabara kuu ya Arusha-Nairobi na ni zaidi ya dakika 90 kaskazini mwa Arusha kwa daladala. Kambi ya Safari ya Robanda iko nje tu ya mbuga ya Serengeti. Kuna idadi kubwa ya wanyama, kwa mfano nyumbu, pundamilia, tembo na twiga. Aina ya wanyama wengine ni pamoja na simba, fisi, swala, topi na nyati.

Usafiri

Mji wa Arusha una Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro kinachopatikana kilomita 60 mashariki ukielekea Moshi kwa ajili ya wasafiri wa kimataifa. Kuna ndege za kimataifa na za ndani. Uwanja wa ndege wa Arusha ni uwanja mdogo magharibi mwa mji, kwa sasa wanaendelea na upanuzi wa uwanja huu. Uwanja huu una abiria 87,000 kila mwaka licha ya udogo wake.

Hakuna huduma za treni ya abiria kutoka Arusha, lakini kuna makochi (mabasi) ya kwenda Nairobi, Dodoma na Dar Es Salaam pamoja na miji mingine ndani.

Tamaduni

Arusha ni mji mzuri kutokana na muziki pia. Hip-hop ya Tanzania inayoita Bongo Flava kwa sasa ni maarufu katika soko la vijana. Inaimbwa katika lugha ya Kiswahili, na ina athari ya muziki wa Waafrika wa Marekani. Mfano mzuri ni X Plastaz, waimbaji Nakaaya, Watengwa Waturutumbi n.k.

Arusha ni makazi makuu ya sherehe nyingi na sikukuu za Tanzania na tamasha la kila mwaka. Wadhamini wa kampuni mbalimbali husimamia tamasha nyingi kila mwaka. Wasanii kama Shaggy na Ja Rule ni wachache tu kati ya wasanii maarufu waliofanya tamasha katika mji huu.

Kila mwaka maonyesho ya Nanenane hufanyika Arusha. Haya huwa maonyesho ya kilimo ambayo wakulima na wafanyabiashara huja pamoja kwa maonyesho, tamasha na burudani. Watu zaidi ya nusu milioni huhudhuria maonyesho haya kila mwaka.

Shule na vyuo vikuu

Kuna shule nne za kimataifa ndani na katika maeneo ya Arusha: Shule ya kimataifa ya Moshi (Arusha), Shule ya kimataifa ya Arusha, Braeburn School, na Shule ya Kimataifa ya St Constantine [4] Shule ya kimataifa ya Moshi ilianzishwa mwaka 1969 na sasa ina wanafunzi 460 kutoka mataifa 46.

Shule ya St Jude hutoa elimu ya bure kwa watoto kutoka familia za kimaskini sana.

Kuna vyuo vikuu viwili. Chuo Kikuu cha Arusha kilianzishwa mwaka 1986 na sasa kina wanafunzi 200 wa kutwa, na hutoa kozi za awali kutoka chekechea hadi darasa la 10. Gredi K-10 kufuata International Baccalaureate mpango wa miaka ya Msingi (PYP) na mpango wa miaka ya Kati (MYP) mitaala kwa maoni ya Afrika na kimataifa. Imekuwa moja ya shule za kimataifa za Ib World tangu 2007.

Chuo cha Arcadia hutoa shahada na pia mihula ya muda mrefu na mipango ya majira ya Tanzania, pamoja na mipango ya kuhitimu na kusoma katika Kituo cha Utafiti cha Nyerere kwa ajili ya amani.

Michezo

Timu ya kitaifa ya mchezo wa raga Tanzania hucheza mechi zake za kimataifa mjini Arusha. Michezo ya 2007 Castel Beer Trophy ilifanywa katika mji huu.

Arusha FC hucheza katika Uwanja wa kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid, huwakilisha mji katika ligi ya mpira wa miguu ya Tanzania.

Miji ndugu

Tazama pia

Viungo vya nje

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:

3°22′S 36°41′E / 3.367°S 36.683°E / -3.367; 36.683

Marejeo

  1. "Halmashauri ya Jiji la Arusha". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Septemba 2022.
  2. "Ripoti ya Sensa 2012" (PDF) (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 2022-03-26. Iliwekwa mnamo 2022-07-03.
  3. https://www.nbs.go.tz
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-09-24. Iliwekwa mnamo 2010-07-21.
  Kata za Wilaya ya Arusha mjini - Tanzania  

Baraa | Daraja II | Elerai | Engutoto | Kaloleni | Kati | Kimandolu | Lemara | Levolosi | Moivaro | Moshono | Muriet | Ngarenaro | Olasiti | Olmoti | Oloirien | Osunyai Jr | Sakina | Sekei | Sinoni | Sokon I | Sombetini | Terrat | Themi | Unga Ltd


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Arusha bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Arusha (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.