Etihad Airways (Kiarabu: الإتحاد‎, ʼal-ʻitiħād) ni ndege kuu ya mji wa Abu Dhabi iliyoanzishwa mnamo 2003.

Inasafiri nchini Mashariki ya Kati, Ulaya, India, Amerika Kaskazini, Afrika, Asia na Australia. Makao yake makuu ni katika uwanja wa ndege wa kimataifa ya Abu Dhabi. Mwaka wa 2008, ilibeba wasafiriwa zaidi ya milioni sita.

Historia

hariri
 
Etihad Airways Airbus A340-500 ikiruka kutoka uwanja wa ndege wa London Heathrow

Etihad Airways ilitangazwa na Sheikh Khalifa in Zayed Al Nahyan kuwa ni ndege ya kitaifa ya nchi ya United Arab Emirates mnamo Februari 2003. Pesa za kuanzia kampuni hii ilikuwa takriban dirhamu milioni 500. Mnamo 12 Novemba 2003 Etihad ilianza kusafiri hadi mji wa Beirut.

Miji inayosafiria

hariri
 
Etihad Airways Airbus A330-200 (A6-EYB) ikishuka kwenye uwanja wa ndege wa London Heathrow
 
Etihad Airbus A330-200 kwenye uwanja wa ndege wa Frankfurt

Ndani ya ndege

hariri

Diamond Zone

hariri

Viti vyake huweza kugeuzwa na kuwa kama kitanda cha urefu wa 6'8". Kuna taa ya kusomea, runinga, kioo, na hata chombo cha kukandia mwili.

Pearl Zone

hariri

Viti huweza kulazwa kama vitanda vya urefu wa 6'1". Kila kiti kina taa ya kusomea pamoja na chombo cha kukandia.

Coral Zone

hariri

Viti huweza kulazwa hadi inchi 33 tu. Kuna huduma ya simu pia.

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri