Jimbo Kuu la Tabora
Jimbo Kuu la Tabora (kwa Kilatini "Archidioecesis Taboraënsis") ni mojawapo kati ya majimbo 34 (2012) ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Chini yake kuna kanda ya Kanisa yenye majimbo yafuatayo: Kahama, Kigoma, Mpanda na Sumbawanga.
Kanisa Kuu liko jijini Tabora, na linaitwa la Mt. Teresa.
Askofu mkuu wake ni kardinali Protase Rugambwa.
Historia
hariri- 11 Januari 1887: Kuanzishwa kwa Apostolic Vicariate ya Unianyembé kutokana na Apostolic Vicariate ya Tanganyika
- 31 Mei 1925: Kupandishwa cheo kuwa dayosisi
- 25 Machi 1953: Kufanywa jimbo kuu
Uongozi
hariri- Maaskofu wakuu
- Protase Rugambwa (tangu 10 Novemba 2023)
- Paul R. Ruzoka (25 Novemba 2006 - 10 Novemba 2023)
- Mario Epifanio Abdallah Mgulunde (9 Machi 1985 – 14 Machi 2006)
- Marko Mihayo (21 Juni 1960 – 9 Machi 1985)
- Cornelius Bronsveld, M. Afr. (25 Machi 1953 – 21 Desemba 1959)
- Maaskofu
- Cornelius Bronsveld, M. Afr. (31 Mei 1950 – 25 Machi 1953)
- Joseph Trudel, M. Afr. (25 Aprili 1933 – 1949)
- Edouard Michaud, M. Afr. (29 Novemba 1928 – 24 Machi 1932)
- Henri Léonard, M. Afr. (27 Juni 1912 – 23 Julai 1928)
- Vicar Apostolic wa Unianyembé
- Askofu François Gerboin, M. Afr. (28 Januari 1897 – 27 Juni 1912)
Takwimu
haririEneo la jimbo kuu lina kilometa mraba 76,151, ambapo mwaka 2004 kati ya wakazi 1,426,998, Wakatoliki walikuwa 257,390 (sawa na 18%) na kuunda parokia 22.
Mapadri ni 64, ambao kati yao 43 ni wanajimbo na 21 watawa. Hivyo kwa wastani kila mmojawao anahudumia waamini 4,021.
Viungo vya nje
hariri- Giga-Catholic Information
- Catholic Hierarchy Informationl
- [1] Ilihifadhiwa 14 Julai 2014 kwenye Wayback Machine. katika tovuti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
- Hati Quemadmodum ad Nos, AAS 45 (1953), uk. 705
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Kuu la Tabora kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |