Singapuri

sinia
(Elekezwa kutoka Singapura)

Singapuri ni nchi ndogo katika Asia ya Kusini-Mashariki.

Republik Singapura
新加坡共和国
சிங்கப்பூர் குடியரசு

Jamhuri ya Singapuri
Bendera ya Singapuri Nembo ya Singapuri
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Majulah Singapura
(Kimalay: "Mbele Singapuri")
Wimbo wa taifa: Majulah Singapura
Lokeshen ya Singapuri
Mji mkuu Jiji la Singapuri1
1°17′ N 103°51′ E
Mji mkubwa nchini Jiji la Singapuri1
Lugha rasmi Kiingereza, Kimalay, Kichina cha Mandarin, Kitamil
Serikali Jamhuri, Serikali ya kibunge
Tharman Shanmugaratnam
Lawrence Wong
Uhuru
Tangazo (Kutoka Uingereza)
Kama jimbo la Malaysia
kutoka Malaysia
31 Agosti 1963
16 Septemba 1963
9 Agosti 1965
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
734.3 km² (ya 190)
1.444
Idadi ya watu
 - 2022 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
5,637,000 (ya 115)
4,117,700
7,804/km² (ya 2)
Fedha Singapore Dollar (SGD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
SST (UTC+8)
not observed (UTC+8)
Intaneti TLD .sg
Kodi ya simu +652

-

1 Singapore is a city-state.
2 02 from Malaysia.


Ramani ya Singapuri

Jiografia

hariri

Eneo lake ni kisiwa kwenye ncha ya kusini kabisa ya Rasi ya Malay pamoja na visiwa vidogo vya kando. Kisiwa kimetenganishwa na bara kwa mfereji mwembamba wa Johor.

Kuna mji mmoja tu: ni jiji la Singapuri lilipopo kisiwani, hivyo huhesabiwa pia kati ya dola-miji.

Historia

hariri

Kisiwa kiliwahi kuwa na makazi mbalimbali katika historia. Mji wa kisasa ulianzishwa mwaka 1819 na Waingereza kama kituo cha biashara ikawa bandari muhimu ya eneo.

Uingereza uliipa uhuru kama sehemu ya shirikisho la Malaysia. Lakini matatizo ya kuelewana yalionekana haraka kati ya wanasiasa Wamalay wa bara na wenzao Wachina wa kisiwani.

Mwishowe Singapuri ikafukuzwa katika shirikisho ikawa nchi ya kujitegemea tarehe 9 Agosti 1965. Mwanasiasa Lee Kuan Yew alikuwa waziri mkuu wa kwanza akaendelea na cheo hiki hadi mwaka 1990 akaongoza Singapuri kuwa kati ya mataifa matajiri ya Asia.

Wakazi

hariri

Kati ya wakazi milioni tano na nusu walio wengi (74.3%) ni wa asili ya China. Mababu wao walihamia huko wakitafuta kazi bandarini.

Wengine ni wakazi asilia Wamalay (13.5%) na Watamil na wengineo waliotokea Uhindi (9%).

Kuna lugha 24 ambazo huzungumzwa nchini Singapuri. Lugha rasmi ni Kiingereza (48.3%), Kichina (38.6%), Kimalay (9.2%) na Kitamil (2,5%).

Upande wa dini, 31.1% ni Wabuddha, 18.9% ni Wakristo, 15.6% ni Waislamu, 8.8% ni Watao, 5% ni Wahindu.

Uchumi

hariri

Uchumi wa Singapuri unategemea zaidi biashara, hasa benki pamoja na viwanda.

Imekuwa kitovu cha uchumi na biashara kwa Asia ya Kusini.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Taarifa za jumla
Biashara
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Singapuri kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.