Guinea Bisau
Gine-Bisau (Kiingereza: Guinea-Bissau) ni nchi ndogo katika Afrika ya Magharibi.
Jamhuri ya Gine-Bisau | |
---|---|
República da Guiné-Bissau (Kireno) 𞤘𞤭𞤲𞤫 𞤄𞤭𞤧𞤢𞥄𞤱𞤮 (Kifulani) ߖߌߣߍ ߺ ߓߌߛߊߥߏ߫ (Kimandinka) | |
Kaulimbiu ya taifa: Unidade, Luta, Progresso (Kireno) "Umoja, Harakati, Maendeleo" | |
Wimbo wa taifa: Esta É a Nossa Pátria Bem Amada "Hii ni Nchi Yetu Inayopendwa Sana" | |
Mahali pa Guinea Bisau | |
Ramani ya Guinea Bisau | |
Mji mkuu na mkubwa nchini | Bisau |
Lugha rasmi | Kireno |
Iko mwambaoni kwa Bahari Atlantiki ikipakana na Senegal upande wa kaskazini na Guinea upande wa kusini.
Jiografia
haririGuinea-Bisau ni kati ya nchi ndogo sana za Afrika ikiwa na eneo la kilomita mraba 36,125; takriban 22% ni visiwa na bahari. Sehemu ya bara ni tambarare. Funguvisiwa la Bissagos lenye visiwa 77 liko karibu na pwani.
Miji
haririMiji mikubwa zaidi ya Guinea Bisau ni: Bisau (wakazi 492,004), Gabú (wakazi 48,670), Bafatá (wakazi 37,875), Bissorã (wakazi 29,468), Bolama (wakazi 16,216) na Cacheu (14,320).
Historia
haririZamani ilikuwa koloni la Ureno kwa jina la Guinea ya Kireno.
Baada ya uhuru (1973/1974) jina la mji mkuu wake lilishika nafasi ya nchi tawala kuwa Guinea-Bisau kwa kusudi la kuitofautisha na nchi jirani ya Guinea na ile ya Guinea ya Ikweta.
Watu
haririWakazi walikuwa 1,515,000 mwaka 2010, wakati walikuwa 518,000 tu mwaka 1950.
Makabila
haririWaafrika ni 99%: makabila makubwa ni Wabalanta 30%, Wafulbe 30%, Wamanjaca 14%, Wamandinka 13%, Wapapel 7%). Wazungu na machotara ni chini ya 1%.
Lugha
haririPamoja na lugha asilia, 32.1% za wakazi wanasema Kireno ambacho ndicho lugha rasmi na 90.4% wanatumia Krioli maalumu ya Kireno ambayo ni kama lugha ya taifa inayounganisha makabila. Lugha nyingine za kigeni zinazotumika ni Kifaransa (7%), Kiingereza (2.9%) na Kihispania (0.5%)
Dini
haririTakriban 46.1% ni Waislamu (hasa Wasuni), 30.6% wafuasi wa dini asilia za Kiafrika, 18.9% Wakristo (hasa Wakatoliki).
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Abdel Malek, K.,"Le processus d'accès à l'indépendance de la Guinée-Bissau.",In : Bulletin de l'Association des Anciens Elèves de l'Institut National de Langues et de Cultures Orientales, N°1, Avril 1998. – pp. 53–60
- Forrest, Joshua B., Lineages of State Fragility. Rural Civil Society in Guinea-Bissau (Ohio University Press/James Currey Ltd., 2003)
- Galli, Rosemary E, Guinea Bissau: Politics, Economics and Society, (Pinter Pub Ltd, 1987)
- Lobban, Jr., Richard Andrew and Mendy, Peter Karibe, Historical Dictionary of the Republic of Guinea-Bissau, third edition (Scarecrow Press, 1997)
- Vigh, Henrik, Navigating Terrains of War: Youth And Soldiering in Guinea-Bissau, (Berghahn Books, 2006)
Viungo vya nje
hariri- Link collection related to Guinea-Bissau on bolama.net Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.
- Country Profile from BBC News
- Guinea-Bissau entry at The World Factbook
- Guinea-Bissau Archived 11 Juni 2010 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Guinea-Bissau at Encyclopædia Britannica
- Guinea Bisau katika Open Directory Project
- Wikimedia Atlas of Guinea-Bissau
- Key Development Forecasts for Guinea-Bissau from International Futures
- Serikali
- Official website
- Chief of State and Cabinet Members Archived 26 Oktoba 2009 at the Wayback Machine.
- Constitution of the Republic of Guinea-Bissau Archived 25 Julai 2011 at the Wayback Machine.
- Guinea-Bissau: Prime Minister’s fate unknown after apparent military coup – West Africa – Portuguese American Journal
- Guinea-Bissau Holds First Post-Coup Election Archived 26 Juni 2016 at the Wayback Machine.
- Biashara
- Habari
- Afya
- The State of the World's Midwifery – Guinea-Bissau Country Profile
- Jiografia
- Master Thesis Archived 4 Agosti 2015 at the Wayback Machine. about the developing Geographical Information for Guinea-Bissau Archived 2 Agosti 2015 at the Wayback Machine.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Guinea Bisau kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |