Macau
Macau (tamka: Makau; kwa Kichina: 澳門; pinyin: Àomén; Jyutping: Ou3 Mun4) ni eneo dogo la Jamhuri ya Watu wa China lenye utawala wa pekee kwenye pwani ya Bahari ya Kusini ya China.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: (kama China) | |||||
Mji mkuu | -- 1 | ||||
' | (mji ulikuwa na tarafa ndani yake zilizofutwa tangu 2000) | ||||
Lugha rasmi | · Kichina · Kireno | ||||
Serikali Mtendaji mkuu
|
Ho Iat Seng | ||||
Kuanzishwa kwa mji Iliundwa na wenyeji Wachina kutwaliwa na Ureno koloni ya Ureno Mkoa wa pekee wa China |
Tangu karne ya 5 BK 1557 31 Agosti 1862 20 Desemba 1999 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
30.3 km² (--) 0 | ||||
Idadi ya watu - 2015 kadirio - 2011 sensa - Msongamano wa watu |
642,900 (ya 167) 552,503 18,568/km² (ya 1) | ||||
Fedha | Pataca ya Macau (MOP )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
MST (UTC+8) -- | ||||
Intaneti TLD | .mo | ||||
Kodi ya simu | +853
- | ||||
1 Mji mkuu ulikuwa "Cidade do Nome de Deus de Macau" au rasi ya Macau yenyewe; makao makuu ya serikali ya koloni yalikaa kwenye tarafa ya Sao Lorenco. 2 Habari kutoka Direcção dos Serviços de Estatística e Censos (ofisi ya takwimu ya Macau ) |
Hali halisi eneo ni rasi ya Macau pamoja na visiwa viwili vidogo, jumla ni km² 32.9 na kuna wakazi 667,400 (mwishoni mwa mwaka 2018). Msongamano wa Macau wenye watu 21,340 kwa kilomita ya mraba ndio msongamano mkubwa kabisa duniani kote.
Tarehe 23 Oktoba 2018 rais wa China Xi Jinping alizindua rasmi daraja la baharini refu kuliko yote duniani (kilometa 55) linalounganisha Hong Kong, Macau na China bara (mji wa Zhuhai).
Koloni la Ureno
haririMacau ilikuwa kituo cha Ureno tangu karne ya 16 na Wareno wakaikodi tangu mwaka 1670.
Macau kama koloni ilithibitishwa katika Mkataba wa Beijing wa mwaka 1887 kati ya China na Ureno.
Macau kama eneo la pekee la China
haririMwaka 1999 ilirudishwa mikononi mwa serikali ya China lakini kwa hali ya pekee inayofanana na ile ya eneo la jirani la Hong Kong.
Hivyo Macau inaendendelea kuratibu yenyewe mambo yake kwa ndani, lakini madaraka kuhusu usalama, jeshi na siasa ya nje yako Beijing.
Watu
haririWakazi wengi (88.4%) ni Wachina asilia, 1.8% ni Wareno. Kwa kuwa uzazi ni mdogo sana, kuna wahamiaji wengi, hasa Wafilipino (4.6%) na Wavietnam (2.4%).
Lugha rasmi ni Kichina na Kireno. Katika matumizi ya kawaida, Kichina cha Canton kinaongoza (87.5%), na Kiingereza kina waongeaji wengi (2.8%) kuliko Kireno (0.7%).
Upande wa dini, 58.9% wanafuata dini za jadi za Kichina (mchanganyiko wa Ukonfusio na Utao), 17.3% ni Wabuddha au Watao, 7.2% ni Wakristo. 15.4% hawana dini yoyote.
Uchumi
haririUchumi wa Macau hutegemea utalii na hasa michezo ya kamari. Kuna pia viwanda vya nguo.
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- Serikali
- Portal of the government of Macau
- Government Information Bureau
- Macau Yearbook Ilihifadhiwa 14 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Cultural Affairs Bureau
- Gaming Inspection and Coordination Bureau
- Taarifa za jumla
- Macau entry at The World Factbook
- Macau Ilihifadhiwa 7 Juni 2008 kwenye Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Macau katika Open Directory Project
- Macau profile from the BBC News
- Wikimedia Atlas of Macau
- Country Study: Macau from the United States Library of Congress (August, 2000)
- Dr Howard M Scott "Macau"
- Utalii
- Macau Government Tourist Office
- Macau City Guide Ilihifadhiwa 26 Aprili 2009 kwenye Wayback Machine.
- Malezi
- Michezo
22°10′N 113°33′E / 22.167°N 113.550°E
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Macau kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |