Mtakatifu Ireneo

(Elekezwa kutoka Irenaeus)

Mtakatifu Ireneo (130202) alikuwa askofu wa mji wa Lyon nchini Ufaransa.

Mt. Irenaeus, Askofu wa Lyon.

Ametambuliwa tangu kale kuwa mtakatifu kama mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 28 Juni[1].

MaishaEdit

Ireneo alizaliwa yapata mwaka 130.

Alilelewa katika mji wa Smirna (leo İzmir nchini Uturuki), akiwa ni mwanafunzi wa Mt. Polikarpo aliyekuwa askofu wa mji huo baada ya kuwa mfuasi wa Mtume Yohane.

Mwaka 177, baada ya kuhamia Ufaransa, Ireneo alipata upadrisho huko Lyons, na baada ya kutumwa kidogo Roma kama mjiumbe kwa Papa, akinusurika hivyo kuuawa katika dhuluma dhidi ya Wafiadini wa Lyon, aliteuliwa kuwa askofu wa hapo.

Ni muhimu kwa juhudi zake za kupigania umoja wa Kanisa dhidi ya uzushi, akisisitiza umuhimu wa mlolongo wa kitume wa maaskofu, akitoa kama mfano orodha ya wale wa Kanisa la Roma baada ya Mtume Petro. Alidai makanisa yalingane na imani ya Kanisa hilo.

Katika maandishi yake alijitahidi sana kutetea imani ya Kanisa Katoliki inayotegemea mapokeo ya Mitume wa Yesu dhidi ya mafundisho ya Wagnosi yaliyotegemea ujuzi ambao yeyote alidai kuwa nao akianzisha kikundi chake.

Ni wa kwanza pia kushuhudia Injili nne kuwa Neno la Mungu.

Kwa mujibu wa mapokeo, aliifia dini yake mnamo mwaka 200.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

MarejeoEdit

  • (1885) The Ante-Nicene Fathers. Buffalo, NY: The Christian Literature Company. 
  • Eusebius (1932). The Ecclesiastical History, Kirsopp Lake and John E.L. Oulton, trans, New York: Putnam. 
  • Hägglund, Bengt (1968). History of Theology, Gene J.Lund, trans, St. Louis: Concordia Publishing. 
  • Minns, Denis (1994). Irenaeus. Washington, D.C.: Georgetown University Press. ISBN 0878405534. 
  • Payton Jr., James R. Irenaeus on the Christian Faith: A Condensation of 'Against Heresies' (Cambridge, James Clarke and Co Ltd, 2012).
  • Quasten, J. (1960). Patrology: The Beginnings of Patristic Literature. Westminster, MD: Newman Press. 
  • Schaff, Philip (1980). History of the Christian Church: Ante-Nicene Christianity, A.D. 100-325. Grand Rapids, Mich: Eerdmans. ISBN 0802880479. 
  • Tyson, Joseph B. (1973). A Study of Early Christianity. New York: Macmillan. 
  • Wolfson, Henry Austryn (1970). The Philosophy of the Church Fathers: Faith, Trinity, Incarnation. Cambridge, MA: Harvard University Press. 

Viungo vya njeEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.