Jamhuri ya Dominika
Jamhuri ya Dominika ni nchi iliyoko kwenye kisiwa cha Bahari ya Karibi cha Hispaniola na inayopakana na Haiti tu.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Kihispania: Dios, Patria, Libertad ( Mungu, Taifa, Uhuru) | |||||
Wimbo wa taifa: Quisqueyanos valientes | |||||
Mji mkuu | Santo Domingo | ||||
Mji mkubwa nchini | Santo Domingo | ||||
Lugha rasmi | Kihispania | ||||
Serikali | Jamhuri Luis Abinader | ||||
Uhuru Tarehe |
27 Februari 1844 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
48,442 km² (ya 131) 1.6 | ||||
Idadi ya watu - Julai 2020 kadirio - 2010 sensa - Msongamano wa watu |
11,229,403 (ya 86) 9,445,281 231.81/km² (ya 65) | ||||
Fedha | Peso ya Dominika (DOP )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-4) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .do | ||||
Kodi ya simu | +1-809 and +1-829
- |
Hispaniola ni kisiwa kikubwa cha pili cha Antili Kubwa (baada ya Kuba) na iko upande wa magharibi wa Puerto Rico, karibu na Kuba na Jamaica. Wenyeji kwa ajili ya kisiwa chao hutumia pia jina la Quisqueya ambalo ni neno la Kitaino, lugha ya wakazi asilia.
Mji mkuu na pia mji mkubwa ni Santo Domingo (yaani Mtakatifu Dominiko). Jina la nchi linatokana na hilo (Jamhuri ya Mt. Dominiko). Jina hilo wakati mwingine linachanganywa na lile la Dominica ambayo ni nchi nyingine iliyoko katika kisiwa cha Karibi chenye jina kama hilo ila lenye maana ya Siku ya Bwana, yaani Jumapili.
Jiografia
haririUso wa nchi ni wa milima mingi. Safu ya milima ya kati ("Cordillera Central") ina milima; ya juu kabisa katika Karibi yote ni Pico Duarte (m 3,175) na Loma Rucilla (m 3,039).
Hali ya hewa ni ya kitropiki lakini mlimani kuna baridi kali zaidi hadi kufikia chini ya 0°C.
Milima mingine ni:
- safu ya "Cordillera Septentrional" upande wa kaskazini (hadi m 1,249 juu ya UB)
- safu za "Cordillera Oriental" na "Costera del Caribe" katika mashariki (hadi m 736 juu ya UB)
- milima ya "Sierra de Baoruco" katika kusini-mashariki (hadi m 2,085 juu ya UB)
Mito iko mingi lakini si mikubwa, kama vile Higuamo, Romana, Yaque del Norte, Yaque del Sur, Yuna, Yuma, na Bajabonico.
Kati ya visiwa vingi vidogo kuna viwili vikubwa kiasi: Saona na Beata upande wa kusini.
Historia
haririMwanzo na koloni la Hispania
haririKabla ya kuja kwa Wahispania Hispaniola ilikaliwa na Waindio Waarawak wa kabila la Wataino kuanzia karne ya 7.
Kristoforo Kolumbus alikanyaga ardhi ya Amerika mara ya kwanza katika eneo la Jamhuri ya Dominika.
Nchi ilikuwa koloni la Hispania kwa jina "Santo Domingo", ikabaki hivyo hata baada ya Ufaransa kununua theluthi ya magharibi ya kisiwa iliyokuja kuwa Haiti baadaye.
Tangu 1510 Wahispania walianza kuleta watumwa kutoka Afrika kama wafanyakazi kwenye mashamba makubwa, hasa ya miwa.
Wengi walitoroka na kuanzisha jumuiya huru za Wamaroni porini katika milima ya kisiwa.
Hata kama leo zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wote wana damu ya Kiafrika kwa kiasi fulani, watumwa hawakuwa wengi katika Santo Domingo jinsi ilivyokuwa upande wa Haiti chini ya utawala wa Ufaransa. Damu ya Kizungu imechangia zaidi, wakati ile ya Kiindio imechangia kidogo kuliko ya Kiafrika.
Utawala wa Haiti
haririSanto Domingo ilitangaza uhuru wake tarehe 30 Novemba 1821 baada ya kuona Hispania ilishindwa kote Amerika Kusini isipokuwa katika visiwa vya Karibi. Lakini baada ya wiki chache nchi ilivamiwa na jeshi la Haiti ikatawaliwa na Wahaiti kwa miaka 22.
Utawala huo ulionekana kwa wenyeji kama utawala wa mabavuna kuanzia 1838 shirika la siri lilifanya mipango ya kuwa nchi ya pekee tena.
Uhuru tena
haririTarehe 27 Februari 1844, wakati wa mapinduzi katika Haiti, matajiri wa Santo Domingo walitangaza uhuru wa Jamhuri ya Dominika.
Mmiaka iliyofuata Haiti ilijaribu kuvamia nchi mara tano ili kurudisha utawala wake lakini watetezi walishinda.
Kurudi kwa Wahispania
haririKati ya 1861 na 1865 rais Santana alikabidhi Dominika tena kwa Hispania kwa sababu aliamini ya kwamba nchi ilikosa nguvu ya kusimama pekee yake. Lakini raia wengine walipinga kurudi kwa Wahispania na kwa msaada wa kijeshi wa Haiti Wahispania walilazimishwa kuondoka.
Jamhuri ya pili
haririJamhuri ya Dominika iliendelea kuwa nchi dhaifu. Kati ya 1865 na 1879 serikali 21 zilihesabiwa pamoja na matukio ya uasi wa kijeshi 50.
Mwisho wa karne ya 19 rais Ulises 'Lilís' Heureaux alikopa pesa nyingi kutoka benki za Ulaya, lakini kutokana na kushuka kwa bei ya sukari alishindwa kuilipia. Lakini nchi za nje zilidai pesa zilizokopwa.
Utawala wa Marekani
haririTangu Januari 1905 mamlaka ya ushuru ilichukuliwa na Marekani.
Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Marekani ilivamia kisiwa chote cha Hispaniola, kwanza Haiti, halafu pia Jamhuri ya Dominika. Utawala wa Marekani uliendelea hadi 1930.
Udikteta wa Trujillo
haririIlifuatwa na kipindi cha udikteta wa mkuu wa jeshi Rafael Leónidas Trujillo aliyechukua utawala kwa miaka 30 hadi kifo chake tarehe 30 Mei 1961. Alitawala kwa unyama na kupora mali ya umma.
Kipindi cha mapinduzi
haririRais Juan Bosch aliyefuata siasa ya ujamaa alichaguliwa tarehe 27 Februari 1963.
Matajiri na serikali ya Marekani walihofia ya kwamba atafuata mfano wa Fidel Castro nchini Kuba, akapinduliwa kwa msaada wa idara ya ujasusi wa Marekani CIA.
Kipindi cha vita ya wenyewe kwa wenyewe kilifuata hadi Umoja wa Mataifa ulipoingilia kati na kutuma wanajeshi wa kurudisha amani.
Hadi sasa
haririMnamo Juni 1966 Joaquín Balaguer, aliyewahi kuwa makamu wa rais Trujillo, alichaguliwa kuwa rais. Uchaguzi huu ulikuwa na wasiwasi mwingi kama kura za baadaye.
Katika miaka iliyofuata Balaguer alirudishwa hadi 1978. Baada ya vipindi vya marais wengine, Balaguer alirudishwa tena 1986, 1990 na 1994.
Kura za mwisho baada ya Balaguer ziliteua marais Leonel Fernández Reyna, Hipólito Mejía na tena Leonel Fernández Reyna tangu 2004.
Watu
haririWakazi wengi (70.4%) ni machotara; vipimo vya DNA vinaonyesha wengi wametokana na wanaume Wazungu na wanawake Waafrika. Wakazi wenye asili ya Afrika ni 15.8% na wenye asili ya Ulaya ni 13.5%.
Kihispania ndiyo lugha rasmi na ya kawaida katika matumizi ya wananchi.
Wengi wao ni wafuasi wa Yesu Kristo (69.1%) katika Kanisa Katoliki (47.8%), ambalo lilianzisha humo jimbo lake la kwanza katika Amerika nzima, au katika madhehebu mbalimbali ya Kiprotestanti (21.3%). Wamormoni ni 1.1%.
Uchumi
haririTazama pia
haririViungo vya nje
hariri- Serikali
- (Kihispania) Presidency of the Dominican Republic
- Official Country Website Archived 1 Julai 2018 at the Wayback Machine.
- World Bank Dominican Republic
- Taarifa za jumla
- Dominican Republic entry at The World Factbook
- Dominican Republic Archived 5 Julai 2008 at the Wayback Machine. at UCB Libraries GovPubs
- Dominican Republic profile from the BBC News
- Wikimedia Atlas of the Dominican Republic
- Key Development Forecasts for the Dominican Republic from International Futures
- Biashara
- Safari
- Maendeleo
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Dominika kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |