Eswatini
Eswatini (jina rasmi tangu mwaka 2018 ni Umbuso weSwatini; kifupi cha Kiswati: eSwatini[1]; kwa Kiswahili pia: Uswazi) ni nchi ndogo ya Kusini mwa Afrika isiyo na pwani katika bahari yoyote.
Ufalme wa Eswatini | |
---|---|
Umbuso weSwatini (Kiswazi) Kingdom of Swaziland (Kiingereza) | |
Kaulimbiu ya taifa: Siyinqaba (Kiswazi) "Sisi ni ngome" | |
Wimbo wa taifa: Nkulunkulu Mnikati wetibusiso temaSwati "Mungu, Mpaji wa Baraka kwa Waswati" | |
Mahali pa Eswatini | |
Ramani ya Eswatini | |
Miji mikuu | Mbabane (serikali) Lobamba (bunge) |
Mji mkubwa nchini | Mbabane |
Lugha rasmi | Kiswati Kiingereza |
Makabila (asilimia) | 84 Waswati 10 Wazulu 6 wengine |
Imepakana na Afrika Kusini na Msumbiji.
Miji mikuu ni Mbabane na Lobamba.
Historia
haririWakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.
Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.
Waswati walianzisha ufalme wao katikati ya karne ya 18 chini ya Ngwane III; mipaka ya sasa ilikubalika mwaka 1881.
Baada ya vita kati ya Waingereza na Makaburu, Swaziland ilukuwa nchi lindwa ya Uingereza tangu mwaka 1903 hadi 1967.
Chini ya mfalme Sobhuza II aliyetawala kwa muda mrefu sana (1921-1982), Swaziland ilipata uhuru tarehe 6 Septemba 1968.
Siasa
haririEswatini inatawaliwa tangu mwaka 1986 na mfalme Mswati III. Mfalme anapingwa mara nyingi kwa sababu anatumia pesa nyingi kwa ajili yake binafsi ilhali wananchi ni maskini sana. Kwa muda mwingi wa uhuru wa nchi katiba imesimamishwa, na mfalme ametawala peke yake.
Watu
haririWakazi wengi ni wa kabila la Waswati na kuongea lugha ya Kiswati ambacho ni lugha rasmi pamoja na Kiingereza. Shuleni kinafundishwa pia Kireno.
Upande wa dini, 89.3% ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, hasa Waprotestanti, lakini pia Wakatoliki (5%). Wanaoendelea kufuata dini asilia za Kiafrika ni 0.5% na Waislamu ni 1%.
Afya
haririEswatini ni kati ya nchi duniani zilizoathiriwa zaidi na Ukimwi; umri wa wastani unafikia miaka 22 pekee kwa sababu ya vifo vingi (64%) vinavyotokana na ugonjwa huo uliopata 26% ya watu wazima wote.
Tanbihi
hariri- ↑ Swaziland king renames country 'the Kingdom of eSwatini', tovuti ya BBC, iliangaliwa Aprili 2018
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- Government of Eswatini
- Wikimedia Atlas of Eswatini
- The Kingdom of Eswatini – a royal experience, official Eswatini tourism website (richly illustrated, english)
- Eswatini National Trust Commission – Conserving Eswatini's Natural and Cultural Heritage, (very extensive descriptions of history, culture and nature, English)
- The Kingdom of Eswatini's Big Game Parks (website about the three big game parks, english)
- Eswatini entry at World Fact Book
- eSwatini country profile from the BBC News
- Key Development Forecasts for Eswatini from International Futures (IFs)
- Photographs of Swaziland Wildlife – Hlane Royal National Park, Mkhaya Game Reserve
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Eswatini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |