Sao Tome na Principe
Jamhuri ya Kidemokrasia ya São Tomé na Príncipe (kifupi: Sao Tome na Principe) ni nchi ndogo inayoundwa na visiwa vichache vilivyoko katika Bahari ya Atlantiki mbele ya pwani ya Afrika ya Magharibi katika Ghuba ya Guinea. Ilikuwa koloni la Ureno hadi mwaka 1975.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: n/a | |||||
Wimbo wa taifa: Independência total (Uhuru Kamili) | |||||
Mji mkuu | Sao Tome | ||||
Mji mkubwa nchini | Sao Tome | ||||
Lugha rasmi | Kireno | ||||
Serikali | Jamhuri Carlos Vila Nova Jorge Bom Jesus | ||||
Uhuru - Date |
Kutoka Ureno 12 Julai 1975 currency = Dobra | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
1,001 km² (ya 171) 0% (visiwa) | ||||
Idadi ya watu - 2021 kadirio - 2012 sensa - Msongamano wa watu |
223,107 (ya 186) 178,739 199.7/km² (ya 69) | ||||
Fedha | {{{currency}}} (STD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
UTC (UTC+0) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .st | ||||
Kodi ya simu | +239
- |
Eneo lake ni hasa visiwa viwili vikubwa vya São Tomé na Príncipe pamoja na visiwa vidogo kadhaa.
Sao Tome na Principe vina umbali wa km 140 kati yake, vikiwa takriban km 250 na 225 kutoka pwani ya Gabon.
Jiografia
haririVisiwa vyote ni vilele vya milima ambayo ni sehemu ya safu za volkeno zilizokua kuanzia sakafu ya bahari hadi kufikia usoni pake. Volkeno hizi ni zimwe, si hai tena.
São Tomé ndicho kisiwa kikubwa, chenye takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi. Kisiwa hicho kina urefu wa km 48 na upana wa km 32. Kimo cha milima yake hufikia mita 2,024 juu ya UB. Sao Tome iko kaskazini kidogo kwa mstari wa ikweta.
Jina la Sao Tome linamaanisha "Mtakatifu Thomas" kwa sababu Wareno walifika huko mara ya kwanza siku ya Mt. Thomas katika kalenda ya Kanisa Katoliki.
Kisiwa cha pili, jina lake ni Príncipe, yaani "Mfalme mdogo" au "Mwana wa mfalme"; kina urefu wa km 16 na upana wa km 6. Milima yake hufikia mita 927 juu ya UB.
Rolas ni kisiwa kidogo kusini kwa Sao Tome chenye wakazi 200 na mstari wa ikweta unapitia humo.
Historia
haririVisiwa hivyo havikuwa na wakazi hadi vilipogunduliwa na Wareno katika karne ya 15.
Baadaye vilikuwa koloni la Ureno kuanzia karne ya 16 hadi 12 Julai 1975, vilipopata uhuru.
Siasa
haririNchi ilifuata siasa ya chama kimoja tangu uhuru hadi mwaka 1990. Katiba ya 1990 imeruhusu vyama vingi.
Utawala
haririNchi ina mikoa miwili (inayolingana na visiwa viwili) na wilaya saba. Wilaya sita ziko kwenye kisiwa kikubwa cha Sao Tome na ya saba iko Principe.
Miji
haririMiji mikubwa zaidi ni (takwimu za 2005):
- São Tomé: wakazi 56.1670
- Santo Antonio: wakazi 8.239
- Neves: wakazi 7.392
- Santa Cruz: wakazi 6.969
- Trindade: wakazi 6.636
Watu
haririWananchi wana asili mbalimbali, wakiwemo Waafrika, Wazungu, Machotara na Waasia.
Pamoja na lugha rasmi ya Kireno, inayojulikana na 98.4% ya wakazi wote, wengi hutumika lugha za Krioli zinazochanganya Kireno na lugha za Kibantu kama vile Saotomense (wasemaji 70.000), Principense (wasemaji 1.500) na Angolar (wasemaji 5.000).
71.9 % za wakazi ni Wakatoliki, takriban 10.2 % ni Waprotestanti.
Uchumi
haririUchumi wa visiwa ulikuwa hasa mashamba makubwa ya kakao pamoja na kahawa na mazao ya minazi.
Katika miaka ya nyuma akiba za mafuta ziligunduliwa baharini katika maeneo kati ya Sao Tome na Nigeria.
Mwaka 2001 nchi hizo mbili zilipatana kuendelea pamoja na utafiti wa akiba hizo. Kutokana na kazi hizi kuna matumaini ya mapato makubwa wakati ujao.
Tazama pia
haririViungo vya nje
haririSerikali
hariri- Presidência da República Democrática de São Tomé e Príncipe - Jamhuri ya kidemokrasia ya São Tomé na Príncipe (makala rasmi, Ureno)
- Assembleia Nacional de São Tomé e Príncipe Ilihifadhiwa 28 Julai 2005 kwenye Wayback Machine. -Baraza la Taifa ya São Tomé na Príncipe (makala rasmi, kireno)
- Instituto Nacional de Estatística Ilihifadhiwa 13 Novemba 2009 kwenye Wayback Machine. - Chuo cha Taifa cha statistikia (kireno)
- São Tomé and Príncipe Government & Political Resources Page
Habari
haririUchambuzi
hariri- BBC News - Country Profile: Sao Tome na Principe
- (kitabu cha wadadisi wa Marekani) - Sao Tome na Principe Ilihifadhiwa 9 Mei 2007 kwenye Wayback Machine.
Utalii
hariri- Agensia ya Usafiri (wenyeji) Navetur-Equatour [1] Ilihifadhiwa 19 Aprili 2017 kwenye Wayback Machine.
Mazingira
hariri- Wahifadhi mazingira guba la Guinea Ilihifadhiwa 10 Aprili 2020 kwenye Wayback Machine.
Mambo mengine
hariri- Article on recent politics: [2] Ilihifadhiwa 13 Oktoba 2008 kwenye Wayback Machine.[3]
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Sao Tome na Principe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |