Komori

nchi huru iliyo kwenye visiwa katika Bahari ya Hindi karibu na pwani ya mashariki ya Afrika
(Elekezwa kutoka Visiwa vya Ngazija)

Komori au Visiwa vya Ngazija (Kifaransa: Comores) ni nchi huru kwenye funguvisiwa katika Bahari Hindi upande wa Mashariki wa Afrika. Iko katika Mlangobahari wa Msumbiji kaskazini kwa Madagaska na mashariki kwa Msumbiji.

Umoja wa Komori
Udzima wa Komori (Kikomori)
Union des Comores (Kifaransa)
جمهورية القمر المتحدة (Kiarabu)
Kaulimbiu ya taifa:
Unité – Solidarité – Développement (Kifaransa)
وحدة، تضامن، تنمية (Kiarabu)
"Umoja – Mshikamano – Maendeleo"
Wimbo wa taifa:
Udzima wa ya Masiwa (Kikomori)
"Umoja wa Masiwa"
Mahali pa Komori
Mahali pa Komori
Ramani ya Komori
Ramani ya Komori
Mji mkuu
na mkubwa nchini
Moroni
11°42′ S 43°15′ E
Lugha rasmi
SerikaliJamhuri ya shirikisho
 • RaisAzali Assoumani
Uhuru kutoka Ufaransa6 Julai 1975
Eneo
 • Eneo la jumlakm2 2 235[1]
Idadi ya watu
 • Kadirio la 2023888 378[1]
Pato la taifaKadirio la 2023
 • JumlaOngezeko USD bilioni 1.364[2]
 • Kwa kila mtuOngezeko USD 1 377[2]
Pato halisi la taifaKadirio la 2023
 • JumlaOngezeko USD bilioni 3.432[2]
 • Kwa kila mtuOngezeko USD 3 463[2]
Maendeleo (2021)Punguko 0.558[3] - wastani
SarafuFaranga ya Komori
Majira ya saaUTC+3
(Afrika Mashariki)
Upande wa magariKulia
Msimbo wa simu+269
Msimbo wa ISO 3166KM
Jina la kikoa.km

Jina limetokana na lugha ya Kiarabu ambapo Juzur al-Qamar (جزر القمر) linamaanisha "visiwa vya mwezi".

Katika Afrika iko kati ya nchi tatu ndogo kabisa.

Jiografia

hariri

Komori ina visiwa vitatu vikubwa: Ngazija, Anzwani, na Mwali. Visiwa vya Mayote ni sehemu ya funguvisiwa kijiografia lakini kisiasa ni sehemu ya Ufaransa kwa sababu wakati wa kupata uhuru watu wa Mayotte walitamka kwa kura nyingi (73%) ya kwamba wanataka kukaa na Ufaransa. Lakini Komori inadai ni sehemu ya eneo lake.

Komori ni sehemu ya bara la Afrika. Ina pia visiwa mbalimbali vidogo.

Hali ya hewa ni ya kitropiki. Kuna mvua miezi yote.

Kitovu cha kisiwa kikubwa zaidi (Grande Comore) ni mlima wa volkano hai Karthala wenye mita 2,461 juu ya UB. Safari iliyopita Karthala ililipuka mwaka 1977 ikaharibu kijiji kimoja.

Miji mikubwa ni (wakazi mwaka 2005): Moroni 42.872, Mutsamudu 23.594, Fomboni 14.966, Domoni 14.509 na Tsimbeo 11.552.

Historia

hariri

Visiwa vya Komori vimekaliwa na watu mbalimbali kutoka Afrika na Asia Kusini katika historia ndefu. Wanaakiolojia walitambua mabaki ya makazi ya watu kutoka karne ya 6 kwenye kisiwa cha Anzwani lakini haijulikani kama watu walitangulia kufika mapema bila kuacha mabaki ya kutambulika.

Waswahili wa kwanza walifika kama sehemu ya uenezi wa Wabantu tangu karne ya 9 BK.

Kipindi cha kwanza huitwa kipindi cha Dembeni (karne ya 9 - 10) ambako Waswahili walianzisha kijiji kimoja katika kila kisiwa.

Wakati wa karne ya 11 hadi ya 15 biashara iliongezeka na Madagaska pia na wafanyabiashara kutoka Uarabuni. Vijiji vidogo vikaongezeka na vijiji vya awali vikakua vikawa miji.

Kumbukumbu ya wenyeji hutaja mara nyingi majina ya Waarabu kutoka Yemen na Saba' kama mababu wa koo asilia lakini hakuna uhakika kama kumbukumbu hizo zinalingana na historia halisi.

Athira ya Kiarabu na ya Kiislamu ikaongezeka kutokana na biashara ya watumwa, dhahabu na pembe za ndovu kati ya Afrika ya Mashariki na nchi za Kiislamu.

Waarabu na Waajemi walijenga vituo kwa ajili ya biashara yao pamoja na misikiti na kueneza dini ya Uislamu kwenye visiwa.

Hata kama Komori si karibu sana na pwani, hata hivyo kutokana na mwendo wa upepo ni kituo muhimu cha jahazi kwenye safari kati ya Kilwa na Msumbiji iliyokuwa bandari kuu ya dhahabu ya Zimbabwe.

Kufuatana na katiba ya uhuru ya mwaka 1975 Komori ilitangazwa kuwa jamhuri ya Kiislamu. Serikali zilipinduliwa mara kwa mara na wanajeshi au na mamluki.

Katiba mpya ya mwaka 2001 imeondoa tabia ya kidini ya dola na iliunda utaratibu wa urais kuzunguka kati ya visiwa vitatu vikubwa.

Katika muundo huo rais wa jamhuri atateuliwa kila baada ya miaka minne kutoka kisiwa tofauti.

Katika uchaguzi ya mwaka 2002 rais Azali Assoumani alichaguliwa kutoka kisiwa cha Ngazidja (Komori Kuu). Katika uchaguzi wa 2006 rais amechaguliwa kati ya wagombea kutoka kisiwa cha Anjouan. Wananchi wa Anjouan walipiga kura ya kwanza. Wagombea watatu wenye kura nyingi wameteuliwa na kusimamishwa mbele ya wapiga kura wa visiwa vyote watakaomchagua rais wa jamhuri.

Rais wa mwaka 2010 alitoka katika kisiwa cha Moheli, baadaye tena rais kutoka Ngazidja, n.k.

Katika uchaguzi wa 2010 ndiye Ikililou Dhoinine aliyepata kura nyingi.

Watu wa Komori ni mchanganyiko wa Waarabu, Wamadagaska, Waafrika wa bara ambao mababu walikuwa watumwa, Wahindi na Wazungu kadhaa.

Kutokana na uhaba wa ajira Wakomori wengi wamehamia nje, hasa Madagaska.

Wakazi wengi ni Waislamu (98%, hasa Wasuni), wakifuatwa na Wakristo (2%). Karibu nusu ya wananchi wote hawajui kusoma.

Ina lugha rasmi tatu ambazo ni Kifaransa, Shikomor (inayofanana na Kiswahili) na Kiarabu.

Nje ya Kifaransa, Kiarabu na Kimalagasy Sanifu, kuna lugha tatu za asili ambazo huzungumzwa na Wakomori, yaani Kimwali, Kianzwani na Kingazija ambazo ziko karibu na Kiswahili.

Uchumi

hariri

Komori ni kati ya nchi maskini zaidi duniani. Kilimo, uvuvi, uwindaji na misitu ni misingi ya uchumi wote.

Barabara na mawasiliano ya meli au ndege ni haba, idadi ya watu inakua haraka, elimu ni duni; haya yote yanasababisha kudumu kwa uchumi wa kijungujiko na uhaba wa ajira. 80% ya wafanyakazi wote wanashughulika kilimo.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 "Comoros". The World Factbook (kwa Kiingereza) (tol. la 2024). Shirika la Ujasusi la Marekani. Iliwekwa mnamo 30 Machi 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 "World Economic Outlook database: October 2023 (Comoros)". World Economic Outlook, October 2023. International Monetary Fund. Oktoba 2023. Iliwekwa mnamo 16 Januari 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Human Development Report 2020 The Next Frontier: Human Development and the Anthropocene (PDF). United Nations Development Programme. 15 Desemba 2020. ku. 343–346. ISBN 978-92-1-126442-5. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 2022-10-09. Iliwekwa mnamo 16 Desemba 2020.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

hariri


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Komori kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.