Turkmenistan
Turkmenistan ni nchi ya Asia ya Kati.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: | |||||
Wimbo wa taifa: Wimbo wa taifa huru na huria | |||||
Mji mkuu | Ashgabat | ||||
Mji mkubwa nchini | Ashgabat | ||||
Lugha rasmi | Kiturkmeni | ||||
Serikali | Udikteta Serdar Berdimuhamedow | ||||
Uhuru Ilitangazwa Ilitambuliwa |
27 Oktoba 1991 8 Desemba 1991 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
491,210 km² (ya 53) 4.9 | ||||
Idadi ya watu - Desemba 2020 kadirio - Msongamano wa watu |
6,031,187 (ya 113) 10.5/km² (ya 221) | ||||
Fedha | Manat (Turkmenistan) (TMM )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
TMT (UTC+5) (UTC+5) | ||||
Intaneti TLD | .tm | ||||
Kodi ya simu | +993
- |
Jina limetokana na lugha ya Kiajemi, likimaanisha "nchi ya Waturkmeni".
Imepakana na Afghanistan, Uajemi, Uzbekistan, Kazakhstan na Bahari Kaspi.
Jiografia
haririNchi ina eneo la km² 488,100, karibu sawa na Kamerun.
Sehemu kubwa (80 %) ni jangwa, hasa jangwa la Karakum.
Milima ya Kopet Dag kusini magharibi inafikia kimo cha mita 2,912.
Kati ya mito mikubwa ni Amu Darya, mto Murghab na mto Hari Rud.
Hali ya hewa si baridi sana lakini kuna joto kali wakati wa kiangazi.
Mvua ni chache; zanyesha hasa kati ya Januari na Mei.
Miji muhimu ni Ashgabat, Turkmenbashi (zamani Krasnovodsk) na Dashoguz.
Historia
haririTurkmenistan ilitwaliwa na Urusi tangu mwisho wa karne ya 19 ikaingia hivyo katika Umoja wa Kisovyeti baada ya mwaka 1917 na kuwa jamhuri ndani yake kwa jina la Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiturkmeni hadi mwaka 1991.
Wakati wa kusambaratika kwa Umoja wa Kisovyeti, kiongozi wa chama cha kikomunisti Saparmirat Niyasov akaendelea kushika uongozi akitawala kama rais hadi kifo chake mwaka 2006.
Niyasov alibadilisha utawala wa chama cha kikomunisti kuwa udikteta wake mwenyewe. Akaanza kutumia jina la "Turkmenbashi" (Baba wa Waturkmeni wote) na sanamu zake zikasimamishwa kote nchiniː mara nyingi zilikuwa sanamu za dhahabu hata kama wananchi walikuwa na maisha magumu.
Mapato kutoka gesi na mafuta ya petroli yalimwezesha kuendesha uchumi wa nchi kwa hiari yake bila mabadiliko makubwa jinsi ilivyokuwa kawaida wakati wa anguko la ukomunisti kwingineko.
Zaidi ya nusu ya wananchi walikuwa hawana ajira na kuishi maisha ya umaskini, lakini wanapewa chumvi, umeme na maji bure. Mkate na petroli zinauzwa kwa bei ya chini sana, lakini kuna uhaba wa mara kwa mara.
Baada ya kifo cha Niyasov kamati ya viongozi ilimteua makamu wa waziri mkuu Gurbanguly Berdimuhammedov kuwa rais mpya ingawa kadiri ya katiba mwenyekiti wa bunge alitakiwa kuchukua nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa bunge alishtakiwa mahakamani juu ya makosa fulani na Berdimuhammedov alithibitishwa katika uchaguzi wa tarehe 11 Februari 2007 kwa 89% za kura. Watazamaji walidai kura ilikuwa ya uwongo.
Mwaka 2013 kwa mara ya kwanza ulifanyika uchaguzi wa vyama vingi.
Watu
haririWaturkmeni wenyewe ni 81.8% za wakazi wote, wakifuatwa na Wauzbeki (9.4%), Warusi (2.2%), Wakazaki (1.6%) na Waarmenia (1.1%).
Lugha rasmi na ya kawaida ni Kiturkmeni (72%). Kinafuata Kirusi (12%).
Wakazi walio wengi ni Waislamu; kuna kadirio ya Waislamu asilimia 96.1 kati ya wakazi wote lakini haijulikani ni wangapi wanaofuata kweli dini yao. Wakristo ni 3.6%, hasa Waorthodoksi.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Brummel, Paul (2006). Bradt Travel Guide: Turkmenistan. Bradt Travel Guides. ISBN 978-1841621449.
- Abazov, Rafis (2005). Historical Dictionary of Turkmenistan. Scarecrow Press. ISBN 978-0810853621.
- Clammer, Paul; Kohn, Michael; Mayhew, Bradley (2014). Lonely Planet Guide: Central Asia. Lonely Planet. ISBN 978-1741799538.
- Hopkirk, Peter (1992). The Great Game: The Struggle for Empire in Central Asia. Kodansha International. ISBN 978-1568360225.
- Blackwell, Carole (2001). Tradition and Society in Turkmenistan: Gender, Oral Culture and Song. Routledge. ISBN 978-0700713547.
- Kaplan, Robert (2001). Eastward to Tartary: Travels in the Balkans, the Middle East, and the Caucasus. Vintage. ISBN 978-0375705762.
- Kropf, John (2006). Unknown Sands: Journeys Around the World's Most Isolated Country. Dusty Spark Publishing. ISBN 978-0976356516.
- Rall, Ted (2006). Silk Road to Ruin: Is Central Asia the New Middle East?. NBM Publishing. ISBN 978-1561634545.
- Theroux, Paul (28 Mei 2007). "The Golden Man: Saparmurat Niyazov's reign of insanity". The New Yorker.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Vilmer, Jean-Baptiste (2009). Turkménistan (kwa French). Editions Non Lieu. ISBN 978-2352700685.
{{cite book}}
: CS1 maint: unrecognized language (link)
Viungo vya nje
hariri- Turkmenistan entry at The World Factbook
- Modern Turkmenistan photos
- Turkmenistan Archived 7 Juni 2008 at the Wayback Machine. at UCB Libraries GovPubs
- Turkmenistan katika Open Directory Project
- Turkmenistan profile from the BBC News
- Wikimedia Atlas of Turkmenistan
- Key Development Forecasts for Turkmenistan from International Futures
- Serikali
- Turkmenistan government information portal
- Chief of State and Cabinet Members Archived 14 Januari 2009 at the Wayback Machine.
- Tourism Committee of Turkmenistan Archived 22 Julai 2014 at the Wayback Machine.
- Vingine
- "Chronicles of Turkmenistan". Publication of Turkmen Initiative for Human Rights. Archived 31 Oktoba 2015 at the Wayback Machine.
- The Turkmenistan Project – weekly news and analysis in English and Russian
- Official photo gallery from Turkmenistan and Ashgabat
- daily news and analysis in Turkish English and Turkmen Archived 3 Novemba 2015 at the Wayback Machine.
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Turkmenistan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |